November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia azidi kupigania ukombozi wa mwanamke

 Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Zanzibar

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na sekta binafsi kufanya jitihada za kuhakikisha wanawake wanapata nafasi na kusikika kwenye maamuzi mbalimbali nchini.

Rais Samia amesema hayo leo kwenye mkutano wa wanawake walio katika sekta ya fedha uliofanyika visiwani Zanzibar.

Aidha, Rais Samia alisema ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi ni suala jumuishi na endelevu, hivyo halipaswi kuchukuliwa kama la kimapinduzi au la serikali pekee.

Rais Samia amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha masuala yanayowahusu wanawake ambayo wafanya maamuzi wengine wanaweza wasiwe na uelewa nayo yanapata nafasi kwenye meza ya maamuzi.

Hali kadhalika, Rais Samia alisema pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi, lazima pia kuweka nguvu kubwa katika kuwainua wanawake kiuchumi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wanawake kujipanga na kufikia malengo yao kwa vitendo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Tamasha la Wanawake Sekta ya Fedha ambalo limefanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024. Tamasha hilo limeandaliwa na Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha (TAWiFA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwanamke Initiatives (MIF) pamoja na TIRA
Baadhi ya Wadau wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha (TAWiFA) pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Tamasha la Wanawake Sekta ya Fedha ambalo limefanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA), Kizimkazi, Zanzibar, tarehe 14 Machi, 2024.