Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde ,ametoa agizo kwa viongozi wa chama cha Mapinduzi matawi mpaka kata wafanye mikutano ya kikanuni kwa utaratibu wa chama ili wananchi waeleze kero zao na kuzifanyia kazi.
Mwenyekiti Said Sidde , alisema hayo katika mkutano wa mkuu wa tawi la ccm Zogoali kata ya Zingiziwa wilayani Ilala ambapo katika mkutano huo aligawa kadi za kisasa za electonic na kupokea wanachama wapya.
“Ninaagiza kwa viongozi wa chama cha Mapinduzi kila tawi pamoja na kata mfanye mikutano ya chama na kupokea changamoto mbalimbali za wananchi CCM wilaya waweze kuyafanyia kazi “alisema Sidde.
Mwenyekiti Sidde alisema baadhi ya Kata na mitaa hawafanyi mikutano hivyo kupelekea wananchi kukosa sehemu ya kuwasilisha changamoto zao.
Aidha katika hatua nyingine aliwataka waongeze wanachama wapya sambamba na kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za electonic ili waweze kuvuna wanachama wapya kwa ajili ya jeshi la ushindi katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wajumbe wa mashina na chama wa Zingiziwa kwa kazi ya kujenga chama, Pia alimpongeza Kada Mashaka Hamidu kutoa eneo la kujenga ofisi ya chama tawi la Zogoali, pamoja na Kada wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala SELEMANI KANIKI kwa kusaidia maendeleo ya wananchi Kata ya Zingiziwa
Mwenyekiti Sidde alisema Kada Selemani Kaniki ni kada wa mfano anashirikiana na chama vizuri pamoja na Serikali katika kuleta maendeleo sehemu mbalimbali.
Katika hatua nyingine alizungumzia mgogoro wa ARDHI wa eneo la Ngobedi ambapo alisema kwa sasa Ngobedi ipo wilayani Ilala kata ya Zingiziwa sio Wilaya ya Kisarawe, Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa wapo katika mchakato wa kuweka mipaka .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Zingiziwa Abdrahi Mpate alisema chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Zingiziwa kipo imara kitashinda mitaa yote ya uchaguzi Serikali za mitaa mwaka 2024 na kuunda Serikali pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025.
MWENYEKITI Mpate aliwataka wana CCM kushiriki vikao vya Chama kila wakati kwa kufuata Kanuni,Katiba na kujenga umoja na Mshikamano.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â