Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Mbulu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Regina Ndege amewataka wanawake wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akisisitiza kuchagua viongozi, makini, waadirifu na wachapakazi.
Hayo amebainisha Machi 10,2024 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Kata ya Yaedachini, wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Ndege amesema siyo kila mwanamke au mwanaume anastahili kuwa Kiongozi bali pindi wananchi watakapomuaona mtu wao anayeishi nao , wanamfahamu vizuri, mienendo na tabia yake ndio watakapo mpatia idhini ya kumpa uongozi.
Pia amesema ni vema wananchi wakatafakari kwa kina namna ya kumpata kiongozi sahihi ambaye hato sababisha migogoro katika maeneo yao hasa ukizingatia miaka iliyopita Kata ya Yaedachini kulikuwa na migogoro mingi iliyohusisha wakulima na wafugaji.
Huku mingine mingi katika jamii ya Wawindani na wakusanya matunda ( Wahadzabe) Wanyiramba,Waairaqw na Wabarbaig.
“Mara nyingi kumekuwa na viongozi wala rushwa ndio kumesababisha kuwepo migogoro mingi katika jamii, ikiwemo ya ardhi, mipaka ya kabila moja na kabila lingine, hali inayosababisha kutokuwa na amani na maendeleo katika eneo husika,”.
Wakati huo huo Ndege amekabidhi mashuka 10, katika zahanati ya Kata ya Yaedachini pia ametoa taulo za kike na mipira miwili kwa shule ya sekondari Yaedachini sanjari na kutoa baiskeli kwa watoto watatu katika Halmashauri ya Mbulu mkoani humo.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa