Na Mwandishi wetu, timesmajira
MWENYEKITI wa ACT-Wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amelakiwa kwa Mapokezi Maalum ya Wanachama, Wapenzi na Wafuasi wa Chama hicho pamoja na Wananchi, huko Kisiwani Pemba.
Mapokezi hayo ambayo yameanza Majira ya Asubuhi kwa kuhusisha Matembezi ya Viongozi na Wafuasi wa ACT-Wazalendo, kutoka Machomane hadi Gombani ya Kale, zilipo Ofisi za Uratibu wa Chama hicho, katika Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, yamelenga pia kuitambulisha Safu Mpya ya Uongozi, baada ya Mkutano wao Mkuu wa Uchaguzi wa hivi karibuni.
Othman ambaye ameambatana na Safu yote ya Viongozi Wakuu ambao walichaguliwa hivi karibuni kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT-Wazalendo, uliofanyika Machi 5 – 6 Mwaka huu, Jijini Dar es Salaam, wameendelea kupokelewa kwa Matembezi na Shamra-shamra zikiwemo za Utamaduni na Burdan za Asili, hapa Nchini.
Katika Hafla hiyo ambayo Mheshimiwa Othman na Wenzake wamepata fursa ya kutambulishwa na kusalimiana na Wanachama na wananchi,
Viongozi mbali mbali wamehudhuria, wakiongozwa na Kiongozi wa Chama,Doroth Semu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba