Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kundi la mifungo mingine ipatayo elfu tatu (3000) imehamishwa kutoka mamalaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera Handeni Mkoani Tanga ili kupisha shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo hilo ambalo ni miongoni mwa maeneo ya maajabu ya dunia huku Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini kikiwahakikishia usalama wa mifugo hiyo.
Hayo yamesemwa alfajiri ya leo Februari 23,2024 na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia nchini Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati akitoa taarifa yanamna ambavyo Jeshi hilo lilivyo Imarisha ulinzi wa mifugo ya wananchi waliohama kwa hiari yao kutoka katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Kwenda Msomera Handeni Mkoani Tanga
Kamanda Pasua amebainisha kuwa mifugo hiyo 3,379 ambayo imehamishwa ni kutoka kaya themanini na mbili ambazo zina jumla watu 41 ambao tayari wamehama kwa hiari kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
SACP Pasua amewahakikishia wananchi ambao bado wanaendelea kujiandikisha kuhama kwa hiari yao kuwa Jeshi hilo limeimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi Pamoja na mifugo yao katika Kijiji cha Msomera.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi