Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Kata ya Minazi Mirefu Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Goldlisten Malisa ,ametoa kilio chake kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo kuliomba eneo la wazi la Hali ya hewa lililopo Minazi Mirefu ili wajenge shule ya Msingi kutokana na kata hiyo aina shule.
Diwani Godlisten Malisa alitoa kulio chake hicho katika ziara ya Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo kuangalia miradi ya Serikali ikiwemo eneo hilo la wazi ambalo linaombwa kujengwa shule.
“Tunakushukuru Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo kwa ziara yako kata ya Minazi Mirefu kilio chetu kikubwa wananchi wa Minazi Mirefu atuna shule ya Msingi tunaomba Serikali yetu ya Dkt.Samia Suluhu Hassan, kupitia mkuu wetu wa wilaya utuombee eneo la HALI YA HEWA litumike kwa ajili ya huduma za kijamii tuweze kujenga na shule ya msingi “alisema Malisa.
Diwani Malisa alisema eneo la hali ya hewa limetelekezwa toka mwaka 1984 mpaka sasa tukipata eneo hilo tutaliendeleza kwa shughuli za kijamii.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya chama vizuri na kujenga nchi katika fursa mbali mbali za maendeleo na kiuchumi.
Pia alimpongeza Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,kwa kusimamia miradi ya maendeleo vizuri katika jimbo la segerea ikiwemo sekta ya afya, sekta ya Elimu na miundombinu ya Barabara .
Kwa upande wake Jane Maswala alisema yeye ni mkazi wa Minazi mirefu watoto wa eneo hilo wanasoma shule za mbali wakati wa mvua watoto wanashindwa kwenda shule kutokana na umbali na sehemu zingine vivuko hivyo wanakosa haki yao ya msingi na kupelekea kukosa masomo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alitumia nafasi hiyo kwanza kumpongeza Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Malisa pamoja na viongozi wa chama ambapo alisema kata hiyo ina wakazi zaidi ya 27,000 na watoto zaidi ya 700 wanasoma shule za jirani
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema atakwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kumuomba eneo la HALI YA HEWA liwe Mali ya Halmashauri ya Jiji waweze kujenga shule ya Msingi na huduma zingine za kujamii na HALI YA HEWA waweze kutafutiwa eneo lingine .
Alitumia fursa hiyo pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu sekta ya afya na miundombinu ya Barabara katika wilaya ya Ilala ambapo pesa hizo zimeweza kujenga shule za msingi Barabara na miradi mikubwa ya afya
More Stories
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo