Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Hospitali ya Selian Lutheran Medical iliopo Ngaramtoni Mkoani Arusha imefanikiwa kuzindua Vifaa mbalimbali vya kutibia ambavyo vimegharimu kiasi cha zaidi ya Bilioni Moja.
Akiongea kwenye uzinduzi huo wa vifaa hivyo mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt Amon Marti alisema kuwa uwepo wa Vifaa hivyo utaweza kusaidia kuraisisha wagonjwa Kupata huduma Za afya Kwa uhakika zaidi.
Dkt Marti Alisema kuwa jengo la maabara na mionzi limeweza kukarabatiwa Kwa zaidi ya Milioni 450,jengo la upasuaji nalo limegharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 130, pamoja na kiteketeza taka Ambapo Napo limegharimu Kiasi cha Milioni 80
Dkt alisema kuwa hapo kabla ya vifaa hivyo walikuwa wanafanya kazi lakini uwepo wake sasa ambao ni wa kisasa zaidi utaweza kuraisisha huduma ambazo wanazitoa kwa wagonjwa.
“uwepo vifaa hivi Ni wa kisasa zaidi na tunarajia kuwa na huduma ambayo ni ya kisasa zaidi Ambapo sasa wanufika wakubwa ni wagonjwa na jamii kwa ujumla”aliongeza.
Awali mgeni rasmi Katika uzinduzi huo msaidizi wa Askofu kutoka Katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT)dayosisi ya kaskazini. Godson Abiely Alisema kuwa uwepo wa vifaa hivyo ni hâtua kubwa sana kwenye sekta ya afya.
Alisema kuwa hospitali inapokuwa na vifaa vya kisasa inaweza kuwaraisisha wagonjwa kupata huduma kwa haraka na hata kuweza kuokoa uhai Wao.
“nawapongeza sana uongozi wa Selian lakini hata kanisa kwa ujumla Ambapo kwa kweli mmepiga hatua na mtakomboa afya za wagonjwa pamoja na kuleta mabadiliko ndani ya jamii kwenye sekta ya afya”aliongeza.
Hataivyo aliwataka wataalamu katika sekta ya afya Hasa ndani ya hospitali hiyo kuhakikisha kuwa wanafuta maadili ya taaluma hiyo ya afya Ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku
“leo mmepata vifaaa vya kisasa sana naweza kusema mmepiga hatua kubwa lakini kama hamtaweza kufuata maadili yenu ni wazi kabisa kuwa havitakuwa na msaada,na sio hapa seliani pekee bali hâta kwa hospitali nyingine hata kama wana vifaa vya mabilioni huku wakiwa hawana maadili mazuri ni sawa na bure kabisa”aliongeza
Naye Irene Daniel alisema kuwa vifaa hivyo vitaweza kuwaraisishia kazi tofauti na hapo Awali Ambapo kazi kwa sasa zimeweza kuraisishwa kutokana na kuwa bora na vya kisasa zaidi
“kwa upande wa maabara tunashukuru sana kwa Kuwa vifaa ambavyo vipo ni vya kisasa zaidi na sasa vitatoa majibu yenye uhakika zaidi.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi