Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online Busega
Katika kuadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, Taifa (MNEC), Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu ametoa vitabu vya uongozi na maadili ya chama,katiba na kanuni kwenye Kata zote za Mkoa huo, ili kuwawezesha viongozi ambao wanataka kuomba uongozi ndani ya chama hicho kujua kazi zao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Kata ya Nyaluwande, wilayani Busega,Gungu amesema vitendea kazi hivyo kwa viongozi hao ngazi ya Kata vitawasaidia kufanya kazi zao kwa weledi na kukisaidia chama kutekeleza majukumu yake vizuri.
“Kama mtakumbuka vizuri mwaka jana tukiwa Maswa wakati tunasherekea sherehe kama hizi niliahidi kutoa vitabu hivi kwa Mkoa mzima, leo navikabidhi hapa tukiwa tunasherekea miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM,”ameeleza.
Ameeleza kuwa vitendea kazi hivyo ni nyenzo nzuri kwa viongozi wao kutimiza majukumu yao vizuri pia vitawasaidia hata wale ambao wanataka kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama kujua kazi zao.
Kutokana na hatua ya Mjumbe huyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif ameeleza kuwa vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa chama, kwani vitasaidia kuwajenga viongozi na kuwawezesha kujua majukumu yao.
“Gungu umefanya jambo kubwa sana vitabu hivi vitawasaidia viongozi wetu kuwaimarisha na kuwajenga vizuri kutekeleza majukumu yao naomba nichukue nafasi hii kukupongeza,”amesema Shemsa.
Gungu pia katika maadhimisho hayo alitoa mifuko ya saruji 30 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya CCM Nyaluwande sambamba na kutekeleza ahadi yake ya kutoa mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi ya Zahanati ya Kata ya Shigala wilayani Busega, ambapo wanachi wa Kata hiyo walimuomba kutokana na kukosa ahanati.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa