November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda awataka wananchi wasiwe wanyonge kudai haki

Na George Mwigulu, Timesmajira Online,Katavi

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amewaomba wananchi wa Mkoa wa Katavi kutokuwa wanyonge kwenye kudai haki zao huku akiwaonya watendaji wa serikali kutokuwa na ujasiri wa kudhulumu haki za watu.

Ameeleza hayo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi mkoani humo yakiwemo ya mzozo wa eneo la uchimbaji wa madini dirifu na ufyekaji wa mazao ya mahindi katiwilaya ya Mpanda na mgogoro wa ardhi eneo la Luhafwe wilayani ya Tanganyika.

Makonda akitatua kero hizo February 04, 2024 katika viwanja vya Shule ya msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani hapo ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakita wavumilia watendaji wazembe serikalini ambao hawataki kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha na kupindisha haki.

“Adui wa CCM sio chama cha upinzani bali niwatendaji wazembe na wavivu wasiotimiza wajibu wao kwenye madaraka waliopewa,chama hakiwezi kutoka madarakani kama watendaji wote wa serikali watafanya kazi kwa mujibu wa sheria,taratibu,utu na sio matumbo yao,” amesema Makonda.

Amefafanua kuwa kipaumbele kikiwa ni utu na kumtizama binadamu bila kujali kipato chake,elimu yake,kabila lake na wakasema binadamu wote ni sawa chama hicho kitaendelea kutawala kwa sababu wananchi wanahitaji huduma.

Katibu huyo wa NEC akiwa katika Wilaya ya Tanganyika amesema ziara yake ya kufanya mikutano ina lenga kuwasikiliza zaidi wananchi kuliko kuwahutubia kwa kuwa msingi wa utawala na mamlaka waliyonayo yanatoka kwa wananchi ambao CCM isingekuwa madarakani na kuitwa chama tawala.

Akitatua mgogoro wa eneo la Luhafwe amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika kuunda tume ya watu wasiopungua 20 itakayo jumuisha wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi na wananchi ili kuona njia bora ya kutatua tatizo la umiliki wa ardhi wanaolalamikia wananchi dhidi ya Wilaya.

Katika mgogoro wa mwananchi kufyekewa mahindi hekali 9 na Mtendaji wa Kata ya Mpanda Hotel Wilaya ya Mpanda amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda kuhakikisha wakulima hao wanalipwa fidia ya mazao yao pamoja na viongozi wa manispaa kukaa na Mwenyekiti wa CCM na kamati ya siasa ya Wilaya kuionesha mipaka na sheria.

Awali Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijiji,Seleman Kakoso amesema Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na changamoto za uhaba wa rasilimali watu licha ya kuwa miundombinu bora kwenye elimu na afya lakini bado wanaupungufu wa walimu 1000 kwenye kada ya elimu na watumishi wa afya 200 hususani katika hospitali ya Wilaya kuna watumishi 40 ambao hawatoshelezi kwani kuna baadhi ya hudu ma zinakwama kutolewa.

Kakoso ameomba msukumo wa serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Majalila kwenda Bandari ya Karema iliyotumia kiasi cha bilioni 48 kwenye ujenzi wake.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo utachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwani kwa kiasi kikubwa utaondoa mgogoro wa Tunduma kwa wafanyabisha kuweza kupitisha bidhaa zao kwa njia ya barabara hadi bandarini kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchini.

Mbunge wa Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi amemwomba Katibu NEC kuweka msukumo kwa ajili ya kupatikna fedha kiasi cha bilioni 7 utakaosaidia kukamilika kwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo hadi sasa yanakosekana baadhi ya majengo muhimu kama sehemu ya kuhifadhia maiti.

Kapufi ameomba kuharakisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa grade ya taifa na mradi wa maji wa miji 28 katika Manispaa ya Mpanda ambao utasaidia kuondoa tatizo la upugufu wa huduma hizo zinazozorotesha kasi ya maendeleo.