Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Tawi la Mji Mpya Mnyamani Mery Obeid , amesema chama cha Mapinduzi CCM tawi la Mnyamani mji mpya,wamejipanga vizuri ccm Mwenyekiti wa Serikali za mitaa atakayeshinda ni wa ccm.
Katibu wa CCM mji Mpya Mnyamani Mery alisema hayo katika mkutano mkuu katika madhimisho ya sherehe za CCM kutimiza miaka 47.
“Tawi la ccm mji mpya ccm tumejipanga vizuri nina jeshi la kutosha mimi na jeshi langu tutakukisha ccm inashika dola kwa kuleta Mwenyekiti wa Serikali za mitaa kutoka ccm hivyo alitaka viongozi wa chama hicho tawi la Mji mpya kata Mnyamani kushirikiana pamoja katika kutekeleza Ilani.
Aliwataka viongozi wa chama na Jumuiya kushirikiana kuwa wamoja kuakikisha ccm inashika dola ,ambapo katika madhimisho ya sherehe za ccm mji mpya walipokea wanachama wapya 200 ambao wamejiunga na chama cha mapinduzi CCM.
Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wa chama ngazi ya kata wanampa ushirikiano mkubwa akiwemo Mjumbe wa Kamati ya siasa ya tawi la Mji Mpya ANUARY MLUGU kwa kujitoa kwa ajili ya kujenga chama na mashina ya wakeleketwa amekuwa mstari wa mbele katika kukisaidia chama.
Katibu Mery Abeid alitoa onyo kwa viongozi wa chama na Jumuiya wa mtaa Mji mpya kwa kiongozi yoyote atakaye semea vibaya Serikali ya Dkt ,Samia Suluhu Hassan adhabu kali itatolewa badala yake amewataka viongozi wa chama hicho kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuleta maendeleo.
Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais kwakuleta maendeleo makubwa kuwajengea shule ya Msingi ya kisasa,ofisi ya Mtendaji ya kisasa na kituo cha afya ambapo alisema kwa sasa Mnyamani huduma za kijamii zote zipo.
Diwani Shukuru Dege alisema Serikali mwezi wa April mwaka huu wanatarajia kujenga barabara za ndani za kisasa katika mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji akitaja baadhi ya Barabara hizo,Faru itajengwa kwa fedha za ndani,Barabara ya Kombo na Maruzuku DMDP.
Diwani Shukuru Dege alisema Mnyamani Bonde la Msimbazi wanapoteza fursa kwa wapiga kura sababu ya mafuriko wapiga kura wanaondoka kukimbia makazi hivyo mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji ukianza utaleta neema mitaa hiyo itakuwa na thamani kubwa .
Alisema vivuko vya Mji mpya vitajengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo hivyo wawe wavumilivu kuvuta subira Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli atatatua kero za vifuko vyao kwani mbunge anafanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi wa Mnyamani kwa kuwaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Mnyamani Mbaraka Mwinyimkuu alimpongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maendeleo makubwa ya Mnyamani pamoja na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ambapo sasa hivi wanajivunia sekta ya Elimu, na sekta ya afya .
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â