November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Simiyu yapongezwa kudhibiti mauji

Na. Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa namna ambavyo wamedhibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kutumia mapanga yaliyokuwa yameshamili siku za nyuma Mkoa huo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa hafla ya kutoa vyeti vya sifa na zawadi kwa askari waliofanya vizuri zaidi 2023 ambapo amewataka askari hao walipata vyeti hivyo kuongeza juhudi zaidi katika utendaji wa kazi zao ndani ya Jeshi hilo huku akipongeza kwa namna walivyodhibiti vitendo vya mauaji ilivyo kuwa changamoto kubwa katika Mkoa huo.

Dkt. Yahaya Nawanda ameongeza kuwa askari wa Jeshi la Polisi anapaswa kuwa kioo muda wote na kutenda haki ikiwa ni Pamoja kutoa huduma bora kwa wananchi wanaolitegemea Jeshi hilo huku akiwataka kuishi katika misingi ya Jeshi la Polisi ambao ni nidhamu, haki, weledi na uadilifu wakati wote wanapotoa huduma kwa wananchi.

Pia amewaomba askari hao kuendelea kushirikiana na wananchi wa Mkoa huo huku akitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu Mkoani humo ikizingatiwa Mkoa huo unafursa nyingi za kiuchumi ikiwemo madini.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishina Msadizi wa Polisi ACP Edith Swebe amesema lengo la zawadi hizo kwa askari ni kuwapa moyo na morali ya kazi ya Jeshi la Polisi huku akibainisha kuwa Jeshi hilo katika Mkoa wa Simiyu utaendelea kuwatambua askari wanaofanya vizuri zaidi kazini na kuwapa vyeti vya sifa na zawadi.

ACP Swebe amewataka askari ambao wajapata vyeti vya sifa na zawadi kuongeza juhudi zaidi katika utendaji kazi na kutoa huduma nzuri na sitaiki kwa wananchi wanaolitegemea Jeshi la Polisi katika ulinzi wao na mali.