January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kihenzile atembelea banda la TCAA

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Waziri wa Uchukuzi
David Kihenzile (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir alipotembelea banda la
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kupata maelezo kuhusu
utendaji wa shughuli za Mamlaka pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga
Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Kihenzile ameipongeza TCAA kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Usafiri wa Anga na kuahidi serikali itaendelea kuwekeza katika sekta hii muhimu pia alisisitiza chuo kuendelea kujitangaza zaidi ili kisikike na kuwafikia watu wengi Zaidi ndani na nje ya nchi.