October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtia nia wa kugombea Ubunge katika Jimbo la Isimani, mkoani Iringa, Adestino Mwilinge

Kada kijana CCM kumpunguza kasi Lukuvi jimboni kwake

Na Zuhura Zukheir, TimesMajira Online, Iringa

MBUNGE wa Jimbo la Isimani, William Lukuvu amenza kuupata upinzani ndani Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kada wa chama hicho Adestino Mwilinge kutangaza kutia nia ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kijiji cha Mbuyuni, kada huyo amesema kuwa ameamua kutia nia kwa mijubu wa kanuni na katiba ya chama hicho inavyosema kila mwananchama anahaki ya kuchaguliwa na kuchagua kwa mujibu wa ibara ya 14 (3) na 15 (1).

Amesema kuwa ameamua kutia nia akiwa kijijini kwao kwa lengo la wadau watambue kuwa yeye ni mkazi wa Jimbo la Isimani na anania ya dhati ya kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wanaoishi katika jimbo hilo.

Adestino Mwilinge

Mwilinge ameamua kutia nia baada ya Katibu Mkuu wa CCM Dr Bashir Ally kutangaza wanachama wa chama hicho wanaruhusiwa kutia nia kwa kuwa ni wajibu wao kulingana na katiba ya chama hicho.

Ameongeza kuwa anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuleta maendeleo ya nchi hii katika kipindi hiki cha miaka mitano aliyokuwa madarakani.

Kada huyo aliyehudumu katika chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka kumi na tano akiwa katika uongozi wa nyadhafa mbalimbali katika chama chake.

Mwilinge amesema kwa sasa hawezi kueleza sababu iliyomfanya kuomba ridhaa ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Jimbo la Ismani huku akiahidi kuweka wazi vipaumbele vyake muda utakapofika.

Aidha Mwilinge amesema kuwa wananchama wa chama cha mapinduzi wanawajibu wa kujilinda chama hicho kwa kusimamia vizuri serikali na kusema mambo mazuri yanayofanywa na chama hicho.