November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi wa maji waanza kutekelezwa Kalambo

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Kalambo–Rukwa

Serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira RUWASA imeanza ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la maji wenye thamani ya shilingi billion 1,770,686,091.83 utakao hudumia zaidi ya vijiji 5 na watu elfu kumi na mbili (12000) katika kata ya Mbuluma wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maradi wa bwawa hilo kaimu meneja wa Ruwasa wilayani humo mhandisi Marwa Webiro amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa tuta la bwawa na ujenzi wa utoro wa maji mita 368 na kusema mpaka sasa kazi zilizo fanyika ni pamoja na usafishaji wa eneo sambamba na upimaji wa alama za tuta lenye urefu wa mita 368 na upimaji wa mita za mianguko ya maji.

Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo imefanya ukaguzi wa mradi huo ambapo mkuu wa wilaya ya  Kalambo Lazaro Komba  amesema mradi huo utahudumia vijiji 5 vyenye idadi ya watu 12000  kwa gharama ya shilingi billion moja 1,770,686,091.83.

Awali akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Vitus Nandi licha ya kuipongeza serikali kwa kutoa fedha hizo amewataka maafisa wa idara ya maji kuharakisha mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na kuwawesha wananchi kuendelea kunufaika na huduma ya maji.