November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TEA yawashauri wadau kuzidi kuchangia maendeleo ya elimu

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

MAMLAKA ya Elimu Tanzania
(TEA) imezitaka taasisi, mashirika
ya umma na binafsi, asasi mbalimbali za kiraia, kampuni, watu, binafsi na wadau wote wa Sekta ya Elimu kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha
elimu nchini kwa kuchangia kupitia
mfuko wa Elimu wa Taifa.

Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mkuu TEA , Dkt. Erasmus Kipesha wakati akizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari.

Mkutano huo uliandaliwa na
Msajili wa Hazina Jijini Dar es
Salaam, jana.

Alisema mfuko huo wa Elimu hupokea michango ya rasilimali fedha na vifaa, ambapo michango ya fedha hupokelewa kupitia mfumo wa malipo wa serikali (GePG) au kwa njia zingine za kibenki ambazo ni rahisi na nafuu kwa mchangiaji.

Dkt. Kipesha alisema michango mingine ya vifaa au huduma hupokelewa moja kwa moja na TEA au kusafirishwa kwenye miradi ya elimu kupitia makubaliano maalum na TEA.

Dkt. Kipesha alisema kuanzia mwaka 2019/20 hadi 2023/24 jumla ya michango na ufadhili wa sh. 1,444,284,034 ilipatikana
ikiwemo michango ya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali kama vile TRA, TANAPA, Taasisi ya Asilia Giving inayojihusisha na shughuli za utalii Jijini Arusha na Taasisi ya Flaviana Matata.

Pia Dkt. Kipesha alitaja michango ambayo imetoka kwa wadau mbalimbali katika mfuko huo.

“Michango ya vifaa kutoka kampuni ya Yalin Global company, Taasisi ya SAMAKIBA, Shirika lisilo la kiserikali la Camara Education Tanzania, Shirika la
BR AC Maendeleo Tanzania , Kampuni ya Baobab, Kampuni ya Nissan Tanzania, Kampuni ya sayaru safi pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)”

Alisema utafutaji rasilimali na michango kutoka kwa wadau kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2019/20 hadi 2023/24 Dkt. Kipesha alisema TEA inalo
jukumua kuhamasisha uchangiaji maendeleo ya elimu kote nchini
ambapo kwa mujibu wa sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya mwaka 2001 sehemu ya 12 (1) (a) na (b) mchangiaji ni mtu yeyote anayetoa mchango wa pesa, bidhaa au huduma kupitia mfuko wa Elimu
au kutekeleza mradi kwa uratibu wa mfuko wa Elimu.

Pia alisema mchangiaji anaweza kuwa mtu yeyote anayetoa udhamini au ruzuku kwa wanafunzi Mbali na watoto wake, familia yake au waajiri wake kwa lengo la kuwasaidia kuendelea na elimu kwenye ngazi ya Sekondari na elimu ya juu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi utafutaji Rasilimali na usimamizi wa miradi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
Masozi Nyirenda aliitaja miradi ya elimu ambayo imetekelezwa kwa mwaka 2022/23 hadi 2023/24.

“Maeneo ya kipaumbele katika ufadhili ni ujenzi wa miundombinu ikiwemo mabweni, nyumba za walimu, mabwalo na majiko, kumbi za mihadhara, madarasa, matundu
ya vyoo, maktaba, maabara za
sayansi na ofisi”

“Vifaa vya kufundishia na kujifunza ikiwemo vitabu, vifaa vya maabara, mashine na mitambo, mbalimbali, vitabu vya kiada na zana nyingine za kufundishia
lakini pia upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA na kufunga mitandao”

Mbali na hayo, Nyirenda alisema kupitia mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TE A , Katika mwaka wa fedha 2022/2023, sh. Bilioni 10.99 ziligharamia ufadhili wa miradi 132 ya kuboresha miundombinu ya elimu Katika shule 151 nchini ikiwemo ujenzi wa vyumba 114 vya madarasa katika shule 38 na ujenzi wa maabara 10 za sayansi katika shule 5 za sekondari.

Kwa upande wa ufadhili wa bajeti ya serikali, Nyirenda alisema ujenzi wa nyumba 52 za walimu katika shule 13, shule 7 zikiwa za msingi na shule 6 zikiwa za sekondari lakini pia ujenzi wa matundu 888 ya vyoo katika shule 37 zikiwemo
shule 29 za msingi na shule 8 za sekondari .

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mkutano huo