November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANROADS yapewa mwezi mmoja barabara ya kinyerezi

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

WAZIRI wa Ujenzi na Mawasiliano Innocent Bashungwa, ametoa agizo la mwezi mmoja barabara ya Kinyerezi, Bonyokwa kutokea Kimara kujengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa alitoa agizo wakati alipotembelea Jimbo la Segerea kuangalia miundombinu ya barabara katika ziara yake wilayani Ilala jana mkoani Dar es Salaam.

“Natoa agizo kwa Wizara ya Ujenzi,TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam na Bodi yenu mkae kikao cha haraka mpitishe hii barabara ya Kinyerezi-Bonyokwa kutokea Kimara yenye urefu wa Kilometa saba ndani ya mwezi mmoja ujenzi wake uanze.

Ambao ameeleza kuwa kwa wakati huu wa mvua anataka ipitike na kuwekwa mitaro ikiwemo Mkandarasi kuanza ujenzi wa daraja.

“Naagiza Bodi ya Barabara, TANROADS Mkoa mpitishe barabara ya Kinyerezi Bonyokwa, Kimara na zingine ambazo zimeelekezwa ndani ya mwezi mmoja ujenzi wake uweze kuanza,”amesema Bashungwa.

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli amewataka wananchi wa Kinyerezi, Bonyokwa kutokea Kimara kuwa wavumilivu barabara hiyo inaanza kujengwa Desemba mwaka huu.

Ambapo ameeleza kuwa sasa hivi wameshatoa tangazo Bodi ya Manunuzi ipo katika mchakato wa hatua za mwisho ambapo ameagiza Mwenyekiti wa Bodi TANROADS kuweka kipaumbele Jimbo la segerea.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Ilala Said Sidde ameeleza kuwa Kata ya Bonyokwa kero kubwa ni barabara za ndani hazina lami.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Kamati ya maafa kwa kutoa maelekezo katika ziara yake kuhusiana na wananchi waliopo mabondeni.

Ambapo amewataka watu wasikae mabondeni mvua zinaendelea kunyesha hivyo waliopatwa na mafuriko wajiifadhi kwa ndugu zao na majirani.