November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekta ya Nyuki yazalisha ajira zaidi ya milioni 2

Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha

Imeelezwa kuwa kwa sasa Tanzania imefanikiwa kuzalisha zaidi ya tani 30,000 kwa Huku Ajira milioni 2 zikiwa zimezaliwa ndani ya nchi ya Tanzania

Hayo yameelezwa na Dr Wilfred Marialle Ambaye ni mtafiti Kutoka katika Taasisi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania(TAWIRI)wakati akiongea na vyombo vya habari mapema jana kuhusiana na utafiti wa nyuki lakini pia mandalizi ya Kongamano la 14 la kimataifa na sayansi Ambapo litawakutanisha watafiti, wanasayansi, pamoja na wadau Ambalo linatatarajiwa kuanza jijini Arusha December 6

Dkt Marialle alisema kuwa kupitia kitengo cha utafiti ambacho kipo chini ya TAWIRI wameweza kufanya tafiti mbalimbali na kisha kubaini kuwa sekta ya nyuki ni moja ya sekta Ambayo imeweza kutoa Ajira za moja kwa moja pamoja na zile Ambazo hazionekani

Alifafanua kuwa hali hiyo imeweza kupaisha Tanzania Ambapo mpaka sasa imeshika Nafasi ya pili Huku Ethiopia Ikiwa inaongoza

“tumeshaweza kufanya tafiti mbalimbali Ambapo zimejikita katika kuhakikisha kuwa sekta ya nyuki inakuwa lakini pia ikiwa inaongoza kwa pato la taifa, lakini kuongeza idadi ya ajira”aliongeza Dkt Marialle.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na mafanikio katika sekta ya uzalishaji lakini bado kuna changamoto mbalimbali Ambazo zinaikabili sekta hiyo

Alitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya wafugaji kufuga nyuki kwa kutumia mizinga ya kienyeji ambapo wakati wa kuvuna asali husababisha uchakataji wake kutokukidhi viwango hasa vya soko la kimataifa

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kuwa na vifungashio ambavyo navyo sio vizuri.

Dkt Marialle alisema kuwa pia changamoto nyingine Ambayo ni kubwa ni pamoja na maitaji kwa soko la nje,

Alidai kuwa katika kukabiliana na changamoto Hizo tayari TAWIRI imeshaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa Tanzania inaongoza kwa uzalishaji Mkubwa lakini pia kwenye soko la dunia Asali ya Tanzania iweze Kushika kasi

Alimalizia kwa kusema kuwa bado wafugaji wa nyuki wana Nafasi kubwa sana ya kuweza kuongeza Thamani ya biashara yao lakini kwa sasa ni muimu sana wao pamoja na wadau wengine wahakikishe kuwa wanashiriki katika kongamano ambalo litawashirikisha wadau wengi sana.