Na Mwandishi Wetu, WAMJW,DSM
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya,” amesema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.
“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo,” Alisisitiza Waziri Ummy
Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini