November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yatoa maagizo kituo cha Afya Mnyuzi

Na Yusuph Mussa,Timesmajira Online,Korogwe

MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Tanga Mohamed Salim maarufu Ratco, ametoa hadi Desemba Mosi, mwaka huu Kituo cha Afya Mnyuzi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kiwe kimeanza kutoa huduma.

Pia ameagiza hadi Novemba 30, mwaka huu jengo la Mama na upasuaji (Maternity Combined) kwenye Kituo cha Afya Kerenge kilichopo Kata ya Kerenge Halmashauri hiyo ujenzi wake umekamilika ujenzi wake.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM kutoka Mkoa wa Tanga Mohamed Salim maarufu Ratco (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Dkt. Miriam Cheche (kulia) alipofika kukagua jengo la OPD Kituo cha Afya Kerenge

Alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti alipotembelea miradi hiyo akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tanga ikiwa ni ziara ya kutembelea miradi kwenye halmashauri 11 za Mkoa huo.

“Hadi tarehe moja Desemba, mwaka huu, Kituo cha Afya Mnyuzi kiwe kimeanza kutoa huduma kwani kina muda mrefu hakijaanza kazi huku wananchi wakiwa wanasubiri huduma” amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Mkwakwani kunapojengwa kituo hicho.

Ambao walidai kuwa wanapata shida ya kupata huduma za afya wakati tayari kuna kituo cha afya kijijini kwao ambacho kimechukua muda mrefu kukamilika, hivyo wanaiomba Serikali kukamilisha kituo hicho ili wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Goodluck Mwangomango (kushoto) akitoa maelezo kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (
kutoka Mkoa wa Tanga Mohamed Salim maarufu Ratco (wa pili kulia) baada ya kufika shule ya Sekondari Magoma

“Jengo la mama na upasuaji kwenye Kituo cha Afya Kerenge tunataka likamilike Novemba 30, mwaka huu,tunaamini kazi iliyobaki ni ya umaliziaji hivyo mtamaliza kwa muda huo ,mimi na Kamati ya Siasa Mkoa, tutakuja tena Desemba mosi, mwaka huu kuangalia kweli kituo kimefunguliwa,” amesema Salim.

Akitoa taarifa ya Kituo cha Afya Mnyuzi, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dkt. Miriam Cheche amesema kuwa wanatekeleza mradi huo kwa gharama ya milioni 500, ambapo fedha hizo zimepokelewa kwa awamu mbili.

Ambapo awamu ya kwanza ni milioni 250 kwa ajili ya jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara na kichomea taka huku awamu ya pili ni milioni 250 kwa ajili ya jengo la kujifungulia na jengo la upasuaji, jengo la kufulia na njia maalumu (walkway).

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe William Mwakilema (katikati) akizungumza kwenye shule ya sekondari Magoma kwenye ziara ya Kanati ya Siasa Mkoa wa Tanga

“Ujenzi wa awamu ya kwanza wa jengo la OPD ulianza Novemba 29, 2021 na umekamilika kwa gharama ya milioni 250 ambapo jengo la OPD na jengo la maabara yalikamilika. Hivyo, jengo la kichomea taka halikujengwa kutokana na uhaba wa fedha,”amesema na kuongeza kuwa Dkt. Cheche.

“Februari 23, 2022 halmashauri ilipokea milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mama na upasuaji (Maternity Combined), njia ya watembea kwa miguu na jengo la kufulia, hata hivyo makadirio ya Mhandisi ya gharama za ujenzi huu yalifikia kiasi cha milioni 270, ambapo ukilinganisha na fedha zilizopokelewa, mradi hautaweza kukamilika,”.

Akitoa taarifa ya Kituo cha Afya Kerenge Dkt. Cheche amesema kituo kinajengwa kwa gharama ya milioni 500 ambapo milioni 200 jengo la OPD huku milioni 300 jengo la kujifungulia na upasuaji (Maternity Combined).

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya mkoa huo Ramadhan Omar (katikati) akizungumza na wananchi shule ya sekondari Magoma

“Mradi huu una changamoto ya fundi kuwa na kasi ndogo ya ujenzi upo kwenye hatari ya kutokamilika kwa jengo la kufulia na njia unganishi ya majengo (walkway) kwa sababu gharama za vifaa vya ujenzi ni kubwa, lakini pia eneo hili lina mwamba ambao umekuwa changamoto kwenye uchimbaji wa shimo la choo,” amesema Dkt. Cheche.

Miradi mingine aliyotembelea ni mabweni shule ya sekondari Magoma na Kwagunda, ujenzi wa jengo jipya la utawala Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe linalojengwa Kata ya Makuyuni, na Stendi Kuu ya Mabasi Mombo.

Moja ya mabweni manne yanayojengwa shule ya sekondari Magoma kwa milioni 520