November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katavi kuachana na ufugaji usio na tija

Na George Mwigulu, TimesMajira Online, Katavi.

Serikali ya Mkoa wa Katavi imeendelea kuhamasisha na kutenga maeneo ya ufugaji wa kisasa wa ng’ombe ili kuondoa ufugaji wa mazoea usiokuwa na tija kwenye soko la kimataifa.

Mkoa huo unakadiriwa kuwa na mifungo 953,000 mingi zaidi ya ng’ombe wenye uzani wa uzito unakadiriwa kuanzia Kg 70 hadi Kg 100 ambao ni mdogo ukilinganishwa na ng’ombe kutoka maeneo mengine wanaofunga kisasa wenye uzani wa kg 300 hadi kg 350.

Ofisa Mifungo Mkoa wa Katavi,Zidiel Muhando (kushoto) akimsomea taarifa ya mradi wa BBT Waziri Mkuu Msitaafu Mizengo Pinda

Ofisa Mifungo Mkoa wa Katavi,Zidiel Muhando akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda katika eneo la ujenzi wa mradi wa BBT kwa ajili ufugaji wa kisasa Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda mkoani hapo ameeleza kuwa serikali inafanya jitahada kubwa ya kutoa elimu kwa wafugaji na kuboresha aina ya kisasa ya mifugo tofauti na iliyopo.

Muhando amesema kuwa wafugaji wakiendelea na ufugaji holela hautakuwa na tija licha ya kufurahia kuwa na mifugo mingi kwa mfugaji moja moja lakini mifugo hiyo ni midogo na thamani yake kifedha ni ndogo.

“Mifugo yetu kwa sasa bado ni midogo midogo imekondeana haiwezi kukidhi viwango vya kimataifa vinayotakiwa kupitia mpango wa BBT tunakwenda kuachana na ufugaji huo,”amesema Muhando.

Amesema mpango wa BBT umedhamiria kuanzishwa katika Wilaya ya Mpanda na Tanganyika ambapo Mpanda hekari 20,000 zilitegwa baada ya kutathimini eneo hilo changamoto ingetokea kwa kuwa eneo hilo lina makazi ya watu wengi hivyo kuamua kubadilisha eneo jipya lenye vitalu 10 lenye ukubwa wa hekari 7752.

“Mfumo wa mashamba darasa ya mpango wa BBT tumeanza kuutekeleza ambao unajumuisha vijana na wafugaji wengine watawezeshwa kutapa mafunzo yakuwajengea ufahamu namna bora ya ufugaji hususani wa kuwanenepesha mifungo ili wakidhi viwango vya masoko ya kimataifa” Amesema Muhando.

Waziri Mkuu mstafuu Mizengo Pinda akizungumza umuhimu wa mradi wa BBT utakao kuza sekta ya ufugaji.

Aidha amesema kupitia ujenzi wa mradi huo wamefanikiwa kujenga bwawa kubwa lenye ujazo wa lita 93,000 utakaosaidia kunyweshea mifungo sambamba na kuhudumia mifungo mingine iliyo nje mpango huo.

Katika kukabiliana na tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Katavi serikali imetenga eneo la Hekari 183,000 kwaajili ya wafugaji ikiwa ni sehemu ya kukabilia na tatizo hilo ambalo mara kadhaa migogoro mingi imeshuhudiwa inayohatarisha amani ya jamii.

Waziri Mkuu Mstaafu,Mizengo Pinda baada ya kusomewa taarifa hiyo amesema uanzishwaji wa eneo hilo utatoa tija kubwa kwenye sekta ya ufugaji katika Mkoa wa Katavi ambapo ameshauri utekelezaji wake ufanyike kwa wakati ili kuondokana na ufugaji wa mazoea.

Pinda amesema kuwa ni muhimu kwa vijana wasomi hususani wa Mkoa wa huo kujengewa uwezo kupitia BBT kujishughulisha na ufugaji na asitokee kijana kusema kuwa hana ajira.

” Mambo ya kuzingatia kwenye uhalisia wake katika jamii hii ambayo wako eneo ambalo tumeamua kulitenga kwa ajili ya mradi wa BBT maana mazigira ya kwetu hapa yanaonesha ni bonde zuri sana ambalo ni sehemu ya marisho ya mifungo na ndipo chanzo cha uhakika wa maji yalipo hivyo ni vema ujenzi wa bwawa hili likanufaisha watu,”amesema.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph amesema eneo la ujenzi wa mradi wa BBT Wilaya ya Mpanda ulikuwa ni eneo la Hifadhi ya Taifa ambapo kwa mapenzi yake Rais Samia Suluhu Hassain alitoa hekari zaidi ya 12,000 ikiwa hekari 7000 zimetengwa kwa ajili ya mifungo na hekari 5000 kwa wakulima.

Jamila amesema katika mradi wa BBT kuna baadhi ya wananchi wamevamia eneo hilo hivyo mpango uliopo ni kuwaondoa na kuwapeleka kwenye maeneo mengine.