Na Yusuph Mussa, Timesmajira Online,Kilindi
VIJIJI 64 vya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga vipo kwenye mpango wa utekelezaji wa miradi ya maji unaofanywa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kati ya hivyo, vijiji 17 miradi inaendelea kutekelezwa, vijiji 24 miradi ipo katika hatua za manunuzi, na vijiji 23 inahusisha utafutaji wa vyanzo vya maji kwa kuchimba visima virefu.
Hayo yamesemwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi Mhandisi Alex Odena akiwasilisha taarifa yake kwenye Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
Kwenye taarifa hiyo iliyosomwa na Mhandisi Abdallah Isula, Odena amesema Wilaya ya Kilindi yenye vijiji 102, vijiji 63 vina huduma ya maji, vijiji 39 havina huduma ya maji.
Katika vijiji hivyo 63, vijiji 52 vina mtandao wa mabomba, vijiji 10 vina visima vya pampu za mkono na kijiji kimoja kina kisima kirefu kisichokuwa na mtandao.
Kulingana na skimu zinazofanya kazi, vituo vya kuchota maji (Vilula) vipo 694, maunganisho ya maji nyumbani ni 523, na idadi ya matenki ni 82 yenye ujazo wa kuanzia lita 1,000 hadi 450,000.
Mhandisi Odena amesema, RUWASA Wilaya ya Kilindi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilitengewa bajeti ya zaidi ya bilioni 1.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, ambapo hadi kufikia Juni 2023, wamepokea kiasi cha zaidi ya milioni 643 sawa na asilimia 54.43 ya bajeti hiyo.
“Ili kuboresha huduma ya maji vijijini, katika kipindi cha mwaka 2023/2024, Serikali imepanga kutumia zaidi ya bilioni 3.7 kwa ajili ya kuendelea kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika Wilaya ya Kilindi.
Ameeleza kuwa miradi ya kipaumbele ni pamoja na ukamilishaji wa miradi ya maji Bokwa/Mafulila,Kilindi Asili na Mabalanga, pia ujenzi wa miradi ya maji Diburuma Songe,Kwamaligwa/Gitu, Mkindi, Mgera/Kisangasa pamoja na ,bwawa la maji Msente.
Mhandisi Odena amesema miradi mingine ni ujenzi wa mradi wa Maji Kwaluguru/Negero, ujenzi wa Bwawa la Maji Saunyi (Lombouti), uchimbaji wa visima 23 katika vijiji 23, ujenzi wa machujio ya maji mradi wa maji Jungu/Balang’a, ukarabati wa mradi wa maji Chamtui, ununuzi wa pampu kubwa mradi wa maji Kwediboma na uboreshaji wa huduma ya maji Songe Mjini (Nkama).
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunziÂ
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
10 Best Online Internet Casinos For Real Cash Oct 202