Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanzisha mahusiano na Jiji la Tulsa kutoka Jimbo la Oklahoma nchini Marekani yanayotarajiwa kuimarisha fursa za uwekezaji katika sekta za elimu, afya, mazingira, utalii, kilimo na biashara.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine ameyasema hayo Oktoba 25, 2025 wakati wa ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum yenye lengo la kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji jijini Mwanza.
“Dhamira yetu kubwa ni kuimarisha mahusiano na wenzetu wa Tulsa ili kubadilishana wataalamu, ujenzi wa miundombinu pamoja na kuboresha sekta yenye changamoto katika jamii yetu” amesema Sima na kuongeza;
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea luleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo elimu na afya katika Jiji letu, lakini bado kuna baadhi ya changamoto hivyo mahusiano haya yataongeza nguvu katika kuzitatua” amesema Sima.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum amesema mahusiano hayo yatasaidia kuimarisha fursa za uwekezaji na uchumi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, utalii na kilimo katika majiji yote mawili.
“Tunalenga kuimarisha ustawi wa jamii ya watu wa Jiji la Mwanza kupitia maboresho ya huduma za kiuchumi na kijamii” amesema Bynum.
Mratibu wa Mahusiano ya Miji Dada kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Billy Brown amesema baada ya mahusiano hayo, hatua inayofuata ni kubaini na kutengeneza fursa zenye manufaa kwa jamii ya Jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Awali tulikuwa tukitumia mahusiano haya kuwajengea uwezo watumishi wa Halmashauri, lakini sasa tunaenda mbali zaidi kwa ajili ya kuwa na miradi itakayotekelezwa kwa ajili ya manufaa ya wananchi” amesema Brown.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana amekutana na ujumbe kutoka Tulsa ukiongozwa na Meya Bynum na kumweleza fursa kubwa za uwekezaji zilizopo jijini Mwanza kuwa ni pamoja na utalii, uvuvi wa vizimba na kilimo na kumwahidi ushirikiano katika kuimarisha mahusiano hayo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya majiji hayo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (kushoto) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) akizungumza na ujumbe wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa Marekani (kulia). Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine akizungumza wakati wa ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum akizungumza wakati wa ziara yake jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akizungumza baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na kulakiwa na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya (katikati). Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kulia) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kulia) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kulakiwa na ngoma ya asili ya kabila la wasukuma.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kulakiwa na ngoma ya asili ya kabila la wasukuma.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukisoma bango la ukaribisho katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (wa nne kushoto) akiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tula, George Bynum (wa tatu kushoto) kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo kutoka benki ya NMB.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi