Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo ametoa zaidi ya mil.2 kwa ajili ya kutatua changamoto shule ya msingi Mpuguso Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Fyandomo amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali hususani katika masuala ya kuboresha elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa.
“Nimewiwa kutoa madawati haya 30 ili watoto wetu wasome vizuri”amesema Fyandomo.
Wakisoma risala katika mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Mpuguso wanafunzi hao wamedai shule yao ina upungufu wa madawati 60 ambapo kila dawati linagharimu 75000.
Baada ya Mbunge kutoa madawati 30 sasa shule inakabiliwa na upungufu wa madawati 30 ambapo wadau wameombwa kuchangia ili kupunguza upungufu huo.
Akiongea kwenye mahafali hayo Diwani wa Kata ya Mpuguso, Japhet Mwakagugu mbali ya kuwashukuru wazazi kuchangia madawati amemshukuru Mbunge Suma Fyandomo kusaidia madawati hayo kwani amesaidia kupunguza upungufu uliokuwepo.
“Rais ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nasi tunapaswa kumuunga mkono ili kuwaondolea usumbufu watoto wetu,”amesema Mwakagugu.
Naye Grolia Ngoka Diwani wa Viti Maalum amesema Suma Fyandomo ametoa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto shule ya msingi Mpuguso lakini pia amekuwa akisaidia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Mbeya hivyo anapaswa kuungwa mkono.
Hivi karibuni Suma Fyandomo alizindua taasisi yake ya Suma Ikenda Foundation inayojihusisha na kuwawezesha wananchi kiuchumi na kusaidia watu wenye uhitaji.
Katika uzinduzi uliofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson ambapo aligawa mashine za kukoboa na kusaga nafaka kwa Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya sanjari na vitimwendo,kitanda cha kujifungulia na taulo za kike.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa