NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako, amefungua semina elekezi kwa Wastaafu watarajiwa wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dar es Salaam
Septemba 11, 2023.
Akizungumza
na wastaafu hao kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Profesa Ndalichako aliipongeza
PSSSF kwa kuandaa semina hiyo iliyobeba kauli mbiu isemayo “Wekeza Mafao yako
Sehemu Salama kwa Uhakika wa Ukwasi”.
Alisema
lengo la semina hiyo ni kuwajengea wastaafu wake watarajiwa uelewa na ufahamu
juu ya umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi ya kukuza vipato vyao baada ya
kustaafu ili kuleta tija na uendelevu wa kipato.
“Usia
wangu kwenu ni kuyatumia vyema madini ya elimu mtakayoyapata hapa kwa kushikilia
mambo makuu matatu nayo ni kuwa na mtazamo chanya, kuweka mipango makini na kutimiza
ndoto binafsi baada ya kustaafu.” Alisema Profesa Ndalichako.
Alisema
kustaafu ni wajibu kwa kila mtumishi hivyo hakuna budi kuendeleza maisha mazuri
hata baada ya kustaafu.
Alisema
ni vema mtumishi akatambua kuwa safari ya kustaafu inaanza pale anapoanza
ajira, hivyo ni muhimu kujiandaa kimipango na kifedha ili kufurahia maisha ya
uhuru lakini umakini katika usimamizi wa fedha.
“Matumizi
ya busara ya fedha baada kustaafu ni muhimu zaidi kwani kwa kiasi kipato
kinapungua na nguvu za kufanya kazi zinaenda zikipungua siku hadi siku,” aliasa.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema PSSSF inatarajia kuwa na
wastaafu 11,000 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.
Alisema
Wastaafu watapatiwa mafunzo ya elimu ya uwekezaji katika masoko ya fedha,
taarifa za nyaraka na utaratibu wa kufuata wakati wa kustaafu, kujiandaa
kisakolojia baada ya kutoka kwenye utumishi, umuhimu wa kutunza mazingira
tunayoishi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, na uhalifu wa kimtandao
ambao unawaathiri wastaafu wengi.
“Mfuko
katika kutambua na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi, una mpango wa kutoa mche mmoja wa mti kwa kila
mstaafu wa PSSSF.
“Mpaka
sasa tuna wanachama 739,000 na lengo hapa ni kila mmoja aweze kupanda na
kuutunza mche tutakaompatia pindi atakapofikia wakati w akustaafu.”Alifafanua CPA. Kashimba.
Semina
kama hii ilifanyika mwaka 2021 kwa wastaafu watarijiwa 3700 bara na visiwani na
mwaka huu pia elimu itawafikia wastaafu kwenye mikoa ya Tanzania Bara na
Visiwani, alisema CPA. Kashimba.
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, akizungumza na wastaafu watarajiwa
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa