Na Esther Macha, Timesmajira Online , Mbarali
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa -2023 ndugu Abdullah Shaib Kaim amezindua mradi wa maji wa Kibaoni wilayani Mbarali mkoani Mbeya na kushukuru serikali kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ya maji.
Pia kiongozi huyo amewashukru wadau ambao wameweza kushirikiana na Serikali kutekeleza mradi wa maji wa Kibaoni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa mradi huo wa Kibaoni umejengwa kwa lengo la kuhudumia wananchi wa vijiji viwili vya kibaoni na Ihahi .
Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa mradi huo unakuwa endelevu, wananchi wametakiwa kuendelea kutunza vyanzo vya maji, miundombinu ya maji pamoja na mazingira kwa ujumla .
Sambamba na kuzindua kwa mradi huo, Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 umeweza kutembelea chanzo cha maji cha Itamboleo pamoja na kupanda miti rafiki kwa mazingira ili kuweza kuhifadhi na kulinda chanzo hicho cha maji.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â