Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Precision Air, zimeungana na kuzindua M-Pesa Super App, inayomwezesha mteja wa Precision Air ‘ku book’ na kufanya malipo kwa njia ya simu kwa kutumia App hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa App hiyo, iliyotambulishwa kama ‘Kula pipa, Kwea anga na M-Pesa, Meneja wa Kitengo cha M-Pesa wa Vodacom, Epimack Mbeteni, amesema kupitia App hiyo itamuwezesha msafiri yoyote wa ndege ya Precision Air ‘Ku book’ na kulipia safari yake kwa kutumia simu.
” Haya ni mageuzi, kama ilivyokawaida Vodacom lengo letu ni kuwaleta watu wote kwenye ulimwengu wa kidigital, hivyo leo kwa kuungana na washiriki wetu wawili ambao ni pamoja na Precision na Tripsiri tumeweza kulifanikisha hili”,.
Kwanzia sasa mtu yoyote anaweza kufanya booking ya Precision Air kwa njia ya simu, ili mradi tu awe na smartphone..baada ya kufanya booking pia anaweza akalipia hapohapo safari yake hakuna haha tena ya kwenda ofisini au kwa Mawakala wa Precision Air kila kitu ni kiganjani mwako”, amesema Mbeteni.
Aidha kwa upande wake, Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la precision Air Specioza Rweyemamu, amesema, asilimia 20 itatolewa kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu, Kama punguzo la tiketi ya ndege kwa wateja watakao weka ‘booking’ na kulipia kwa kutumia M-Pesa Super App.
“Leo tunazindua kitu kipya, ambacho ni M-Pesa Super App, hivyo na sisi kama Precision tutatoka discount ya asilimia 20 kwa muda wa miezi mitatu, kwa wateja watakao weka booking na kulipa kwa kutumia App hiyo”, amesema Rweyemamu.
Rweyemamu, ametoa wito kwa Watanzania kuitumia fursa hiyo na kudai kuwa, huduma za kidigital ni nzuri kwani hazihitaji ofisi kwani hata ofisi ikifungwa mtu ataweza kupata huduma kwa njia ya simu.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria