November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Muungano wa Mapinduzi ya kijani AGRA ataka wabia  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kilimo

Na David John timesmajira online

RAIS wa Muungano wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF), Dkt.Agnes Kalibata, amewataka wabia wa Jukwaa hilo kuchukua hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula .

Dkt. Kalibata ametoa rai hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa AGRF .ambapo mkutano huo pia ulimuhusisha Waziri wa Kilimo wa Tanzania Hussein Bashe.

“Tunachotakiwa kuona kutoka kwa wanachama ni kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo,” Dkt. Kalibata amesema.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanajitokeza kama changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo barani Afrika hali inayozidi kutotabirika na isiyo na uhakika ya mifumo ya hali ya hewa katika bara imeweka mzigo wa ziada kwa usalama wa chakula na maisha ya vijijini.

uharibifu mkubwa wa mashamba na nyumba katika mafuriko ya hivi majuzi nchini Burkina Faso na ukame wa muda mrefu nchini Ethiopia, vinaonyesha ukubwa wa tishio linaloletwa na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.

Ameshangaa kuona jinsi nchi za Kiafrika zilifanikiwa kufanya biashara na nchi za nje ya bara lakini zilifanya vibaya katika biashara ya ndani ya bidhaa za kilimo.

“Kwa nini biashara nje inawezekana na si ndani ya  bara? Tunanunua chakula kutoka nje ambacho wakulima wetu wanaweza kuzalisha. tunaweza kuanza kile tunachoweza kufanya, unapaswa kuelewa kuwa sekta hii inaweza kutoa ajira kwa vijana wetu,” amehoji

Kwa upande wake, Waziri Bashe amesema ili wakulima wadogo waweze kuboresha uzalishaji wanahitaji sera na miundombinu bora.

Amebainisha kuwa ushiriki mdogo wa vijana katika kilimo ulitokana na mtazamo ambao umejengwa kwenye simulizi la awali la kilimo ambapo lilihusiana na shughuli ya kuweka chakula mezani.

“Ilikuwa bahati mbaya kwamba suala la uzalishaji mali halijasimuliwa, lilisahaulika,” ameongeza.

pamoja na hatua nyingine zilizochukuliwa na serikali kushughulikia hili ni kuanzisha mpango wa Ruzuku na Mikopo nafuu kwa vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili waweze kushiriki katika usindikaji na ufungashaji wa mazao ya kilimo.

“Vijana wanapoona wenzao katika kilimo wanafanikiwa wangependa pia kujishughulisha, hii ni njia ya kuwavutia katika kilimo,” amesema.

pia amefafanua kuwa AGRF ya 2023 haihusu kujadili kuhusu Uzalishaji Jeni (GMO) katika kilimo, bali inahusu kubadilisha mifumo ya chakula  kutoka uzalishaji hadi sokoni.