Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Mwanamuzuki Khaleed Ramadhan maarufu kama Tunda Man alifanya onyesho la aina yake kwenye shule ya Brilliant na kuzishauri shule ziwe na profamu za kuibua vipaji vya vijana.
Ametoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akitumbuiza kwenye mahafali ya shule ya sekondari ya Brilliant ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Amesema mbali na masomo kuna umuhimu kwa shule kutenga muda wa michezo na burudani kwani kwa kufanya hivyo wataibua vipaji vingi na watu maarufu kwa siku za usoni.
Tunda Man aliibua shangwe kwa wanafunzi wa shule hiyo mara tu mshereheshaji wa tukio hilo alipotangaza uwepo wake kwenye mahafali hayo.
Aliposhuka kwenye gari lake wanafunzi walishindwa kujizuia na wote walivamia katikati ya uwanja na kuanza kuimba naye nyimbo mbalimbali ukiwemo ule wa naipenda Simba hatua uniue mimi sihami.
Tunda mbali na kuimba wimbo maarufu wa naipenda Simba sihami hata mniue aliimba nyimbo mbalimbali za kupongeza mafanikio ya timu ya Yanga hali iliyoibua furaha na shangwe kwa wanafunzi wa timu zote mbili.
Amewataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha nne inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua