Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
MSIMAMIZI wa uchaguzi mdogo Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Missana Kwangura amesema kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika Septemba 19,2023 ili kujaza nafasi ya marehemu Francis Mtega aiiyekuwa Mbunge wa jimbo hilo baada ya kupatwa na ajali julai 1,2023 iliosababisha kifo chake.
Akitoa taarifa Msimamizi huyo wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali Missana amesema taratibu za uchukuaji fomu zilianza Agosti 13,2023 na kukamilika Agosti 19,2023 ambapo vyama 14 vimejitokeza kuchukua fomu lakini chama kimoja hakikurejesha fomu.
Missana amevitaja vyama vilivyochukua fomu kuwa ni pamoja na AAFP, DP, UDP, CCK, UPDP, ACT,TLP,CCM,ADC,NLD,NRA,UMD,ADA TADEA na CHAMA MAKINI chama pekee ambacho hakikurejesha fomu ni NRA.
Baadhi ya wagombea baada ya kurejesha fomu na kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge kila mmoja amejinadi kushinda nafasi hiyo.
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Modestus Kilufi naye ni miongoni mwa wagombea kupitia ACT Wazalendo ambaye ameeleza kuwa bado ana kiu ya kuwatumikia wananchi wa Mbarali kwani kuna mambo mengi hayajapatiwa ufumbuzi.
Naye Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM ,Bahati Ndingo aliyesindikizwa na viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya kwa msafara wa pikipiki na magari kutoka Ubaruku hadi ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali amesema watazisaka kura mlango kwa mlango, uvungu kwa uvungu ili kueleza mambo mazuri yaliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Maneno hayo yameungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali Mary Mbwilo ambaye amesema hana shaka na mgombea wake kwani ni mtu makini na msikivu.
Hussein Msea wa ADA TADEA amesema lengo ni kuhamasisha amani katika nchi huku Halima Magambo wa AAFP amefurahi kuteuliwa na kuahidi kufanya kampeni za haki.
Fatuma Rashid Zania wa NLD amesema yeye kama kijana na mwanamke anasisitiza amani huku Moris Thomas Ngonolo wa TLP amesema amejipanga na chama chake kuhakikisha anashinda uchaguzi.
Hata hivyo Bariki Oswald Manyalu wa Demokrasia Makini ameridhishwa na mchakato mzima uliofanywa na tume kwa kuthamini hata vyama vidogo huku Hashimu Abas ADC amesema kipaumbele chake akichaguliwa ni kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo imekithiri Wilaya ya Mbarali.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nao wamefika Mbarali lengo ni kutoa elimu hususani gharama za uchaguzi.
More Stories
5 “best” Bitcoin Online slots games
Best Web based casinos Norway Your own #1 Norwegian Online casinos 2024
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere