Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam.
KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom kwa kushirikiana na benki ya NMB pamoja na Google wamezindua kampeni ya ‘miliki simu lipa mdogo mdogo’ inayowezesha wananchi wa kipato cha kati kumiliki simu janja (Smartphone).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha kutoka Vodacom, Hilda Bujiku amesema kuwa lengo ni kuwezesha watu wa kipato cha kati kuweza kumiliki simu janja, ambapo awali atatakiwa kulipia kiasi cha Sh.20,000 na baada ya hapo mteja atakuwa akilipia kila siku Sh. 900.
Ameeleza namna ya upatikanaji wa simu hizo kwa mkopo wa gharama nafuu, Hilda amesema, kwa mwaka huu zitatolewa simu milioni 1 kwa wateja ambao watakidhi vigezo vya kuweza kukopeshwa, ambapo zipo simu za aina mbalimbali ikiwepo aina ya Itel special ya nchi tano, inayokopeshwa kwa kianzio cha Sh. 20,000.
Akitolea ufafanuzi wa upatikanaji wa simu hizo za mkopo, Hilda amesema anayehitaji kupata mkopo wa simu hizo lazima awe mteja wa Vodacom kwa maana ya kuwa awe anatumia lakini ya mtandao huo.
Kwa upande wake,Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara kutoka NMB Filbert Mponzi amewataka wananchi wote kutumia fursa hiyo ya kujipatia simu janja kwa mkopo na kudai kuwa lengo la ushirika huo ulioanzishwa na tasisi hizo tatu ni kuwakomboa wananchi wenye kipato cha kati kuweza kumiliki simu janja.
” Muungano huu ni mkubwa kwani ukiangalia NMB ni kubwa na Vodacom ni kampuni kubwa,hivyo kwa wale ambao bado wanatumia vitochi nadhani huu ndo wakati sahihi wa kuweza kujipatia smartphone kwa mkopo wa gharama nafuu kabisa…kwani lengo letu ni wananchi wote twende kidigitali”,amesema Mponzi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi