November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaongeza bilioni.14.5 kuharakisha mradi wa maji Kiwira

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

Serikali kutoa billioni 14 za utekelezaji wa mradi wa maji Kiwira ambao utasaidia kutatua changamoto ya muda mrefu inayowakabili baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya ya upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo mengi.

Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ,Dkt.Tulia Ackson akizungumza na wananchi wa Kata ya Nsalaga kupitia mkutano wa hadhara amesema anatambua maeneo mbalimbali hayana huduma ya maji ikiwemo shuleni na mradi ukikamilika maji yatafika kila sehemu na kutakuwa hakuna mgao.

Dkt .Tulia amesema serikali tayari imekwisha mpata mkandarasi atakayetekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili na changamoto ya maji itafika ukomo.

Pia Dkt. Tulia amewatoa wasiwasi wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuhusiana na mkataba wa bandari kuwa unamaslahi mapana kwa nchi yetu ndio mana Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetupilia mbali malalamiko ya Mawakili wanne wakiongozwa na Boniphace Mwabukusi wa kupinga mkataba huo.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Clemence Mwandemba amemuomba Dkt .Tulia kufikisha ombi kwa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan la kuboresha miu za mitaa zitakazo

Katika hatua nyingine Dkt. Tulia ameahidi kukamilisha ujenzi wa madarasa yaliyoanza kujengwa ambapo kiasi cha millioni 580 zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya Kata ya Nsalaga itakayosaidia watoto kutokutembea umbali mrefu kufuata elimu.