December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Samia atembelea Banda la Benki ya Stanbic maonesho ya nanenane

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi kutoka Stanbic Bank Tanzania (SBT), Omari Mtiga (kulia) akumueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo ya kifedha itakayowawezesha wakulima kupata zana za kisasa za kilimo kwa ajili ya kilimo biashara wakati wa maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya. Aliyesimama pembeni ya Rais (kushoto) ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Abdallah Ulega akizungumza kwenye banda la Stanbic Bank Tanzania (SBT) mara baada ya kujionea huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya fedha hasa zana za kisasa kwa ajili ya kilimo biashara zinazotolewa na benki hiyo wakati wa maonesho ya Nane Nane mkoani Mbeya.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Abdallah Ulega (kulia) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi kutoka Stanbic Bank Tanzania (SBT), Omari Mtiga kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo ya fedha itakayowawezesha wakulima kupata zana za kisasa za kilimo kwa ajili ya kilimo biashara wakati wa maonesho ya Nane Nane mkoani Mbeya.