November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wahimizwa kupata elimu dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

NAIBU Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu amewaasa   watanzania kufika kwenye Banda la Ofisi hiyo katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kupata Elimu dhdi ya ugonjwa wa UKIMWI. 

Nderiananga ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la Ofisi hiyo jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Amesisitiza wananchi waendelee kufika banda la ofisi ya Waziri mkuu, Sera Bunge na Uratibu ili kujifunza zaidi wapate kujua namna ambavyo wanaweza kukabiliana kabla na baada na namna ambavyo serikali inaratibu kuanzia serikali kuu mkoa, wilaya na mpaka ngazi za chini kwenye eneo la maafa.

Aidha amesema Serikali ipo katika hatua za kufanyia tathimini Programu ya Kilimo na Uvuvi ya miaka mitano Ili kuhakikisha nchi inapiga hatua katika sekta hizo.

“Tupo katika hatua za kufanyia tathimini  programu ya miaka mitano  ya kilimo na Uvuvi Ili iweze kuleta tija ya uzalishaji katika sekta hizo kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.”amesema Ummy na kuongeza kuwa

” Wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla waje  wajifunze lakini pia  waone namna taratibu wizara zingine za kisekta katika  kilimo na uvuvi  namna nchi yetu inavyopiga hatua kwa mana hiyo mimi niwakaribishe Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu tuendelee kushirikiana tuendelee kujifunza kazi zinazofanywa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,” amesema Ummy