November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UDSM yaongeza thamani ya mazao

Na Yusuph Mussa, Timesmajira Online, Mbeya

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kupitia idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia katika imeongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa kufanya usindikaji na kuzalisha bidhaa zinazotokana na mazao hayo.

Hivyo kutoa fursa ya kuboresha maisha ya wakulima, kukuza biashara, na kuboresha afya ya watumiaji wa vyakula hasa vya asili.

Crispin Dionice, Mkufunzi Msaidizi katika Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akionesha baadhi ya bidhaa zilizoongezwa thamani katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Hayo yalisemwa Agosti 7, 2023 na Mkufunzi Msaidizi katika Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Crispin Dionice kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dionece amesema wamekuwa wakijitahidi kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa chakula na utapiamlo ambapo jitihada hizo za kuongeza thamani zinalenga kuisaidia taifa katika mapambano dhidi ya njaa, magonjwa, na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia uzalishaji na matumizi ya bidhaa za vyakula.

Ameeleza kuwa miongoni mwa bidhaa zenye thamani ambazo wamefanikiwa kuzalisha ni mafuta ya kupaka ya parachichi kutoka kwenye nyama ya parachichi.

“Bidhaa hii inajulikana kuwa na vitamin E na omega tatu, ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi,mafuta haya husaidia kuponya michubuko midogo, kutuliza ngozi kavu na kupunguza muwasho kwa nywele, husaidia kufanya ziwe laini, zenye kung’aa, na kuzuia kuvunjika,”amesema Dionice.

Emily Mwantisya, mwanafunz Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiuza bidhaa kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye Banda la chuo hicho katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dionice amesema pia mafuta ya kula ya parachichi ambayo yana omega tatu na vitamin E hivyo kuwa na manufaa kwa afya ya moyo na mishipa pia yanaongeza ladha na ubora wa chakula yakitumiwa katika mapishi mbalimbali huku yakiwa na manufaa mengi kwa afya ya ngozi kwa sababu yana vitamini E na antioxidants ambavyo huisaidia ngozi kuepuka madhara ya jua na kuiweka ikiwa na muonekano mzuri.

“Kwa ndani, mafuta ya parachichi husaidia afya ya moyo na kudhibiti cholesterol, husaidia mzunguko wa damu, kupunguza maumivu ya viungo na kuboresha afya kwa ujumla,ni vizuri kutumia kwa kiasi na kushauriana na mtaalamu wa afya kabla ya kuanza, hasa kwa watu wenye matatizo ya afya,”.

Pia amesema unga wa parachichi unatoa njia bora ya kuongeza virutubisho kwenye vyakula unaweza kutumika kama kiungo katika vyakula vingine au kama lishe ya kuongeza thamani katika mchanganyiko wa vyakula.

Huku unga wa senene (makapi), bidhaa hii ina faida za lishe na inaweza kutumiwa kuongeza thamani ya vyakula kwa kuongeza protini na virutubisho vingine vya kimetaboliki.

Crispin Dionice (kulia) ambaye ni Mkufunzi Msaidizi katika Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimuonesha mteja baadhi ya bidhaa zilioongezwa thamani katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mafuta ya senene yanaweza kutumika kama chanzo cha lishe, kuongeza ladha hata kwa madhumuni ya afya, kwani yanaweza kuwa na athari chanya kwa afya ya moyo na mishipa kupunguza cholesterol vilevile yanasaidia kuimarisha kinga ya mwili, kudhibiti sukari, na kutoa virutubisho muhimu kwa mwili.

“Mkate wa senene ambao unatokana na makapi yake baada ya kukamuliwa mafuta, bidhaa hiyo inachanganya ladha ya asili ya makapi ya senene na ngano ikiwa ni njia bora ya kuongeza thamani ya vyakula na kuleta aina mpya za vyakula,”.

Hata hivyo amesema pia kuna biskuti na cookies za senene (makapi na unga wa ngano) ambazo hutoa chaguo bora la kujifurahisha, zikiwa na virutubisho kutoka kwa senene na unga wa ngano.

“Mkate wa chia (mbegu za chia zimechanganywa na ngano),ambazo uwa na protini na nyuzinyuzi nyingi, hivyo mkate huu unakuwa na manufaa kwa afya ya utumbo na husaidia kupunguza uzito uliokithiri huku mkate wa ua la ndizi (unga wa ua la ndizi na ngano), bidhaa hii inatoa fursa ya kutumia rasilimali za ndizi kwa njia mpya na yenye thamani inaweza kuwa na virutubisho vingi kutokana na ndizi,”.

Aidha yogate yenye ndizi,bidhaa hii inaleta pamoja faida za maziwa na ndizi, ikitoa lishe bora kwa afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Dionice amesema hizo ni baadhi tu ya faida za bidhaa zao ambazo wameziongeza thamani, kwani kabla ya hapo, wananchi walikuwa wakikamua mafuta ya senene wanatupa makapi hayo.