Na Esther Macha, Timesmajira, Online,Mbeya
UMOJA wa machifu wa Jiji la Mbeya, wamelaani vikali baadhi ya mamluki wanaojitambulisha kuwa ni machifu na kutoa matamko mbalimbali ya kuipinga serika wakidai kuwa matamko hayo yanawagombanisha na serikali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Machifu Mkoa wa Mbeya, Chifu Rocket Mwashinga wakati akitoa tamko la kupinga upotoshwaji wa taarifa ya uwekezaji wa bandari unaofanywa na baadhi ya watu wanaojiita machifu.
Chief Mwashinga amesema kwamba kuna watu wamejitokeza kuwa wao ni machifu wa Mbeya kuwa hawataki uwekezaji wanataka hao watu au mtu ajitokeze aseme.
“Hilo jambo limetuumiza sana machifu wa Mbeya eti tumeongea kuwa hatutaki uwekezaji huyo muongeaji mwenyewe hatumjui,hatujui anatoka wapi na ni Chifu wa wapi na kila chifu ana himaya yake na kila chifu yupo sehemu yake yeye kwanza ni kabila gani machifu wa mbeya wote hapa ni kabila la Wasafwa uchifu huwezi kwenda sehemu nyingine ukasema ni chifu wakati chifu yupo,”amesema Chifu Mwashinga.
Akizungumzia kuhusu uwekezaji wa bandari Chifu Mwashinga amesema hakuna nchi inafanya peke yake bila uwekezaji wapo watanzania wapo nje wanafanya kazi na wa nje wanakuja Tanzania ndo uwekezaji watu hubadilishana.
“Lakini leo anakuja mtu anasema machifu wa Mbeya wamekataa uwekezaji Chifu gani huyo ameyesema hayo bila kuwekeza serikali itafanyeje uchumi utakuwaje huyo mtu anayejiita chifu sisi tunamkataa kabisaa,”amesema Chifu Rocket Mwashinga.
Chifu George Lyoto amesema kuwa kuna baadhi ya watu hawatambui ambao wanajiita machifu hili jambo ni baya hao wenzetu hatuwajui wa wapi ni himaya zao hatuzijui bali ni kikundi tu kilichojitokeza cha kutaka kuwachafua machifu na sisi machifu katika utawala wetu tunaiunga mkono serikali.
Aidha amesema kwamba wanaunga mkono serikali na kuipa ushirikiano wa kutosha kwasababu ya maendeleo wanayoona kazi yao kubwa ni kuchafua machifu wa Mbeya .
“Tunatoa ushirikiano kwa serikali sababu serikali inawajali na sasa hivi serikali haiwezi kufanya jambo kubwa pasipo machifu wanaojulikana wa Mbeya kujulishwa hivi karibuni tumeshirikishwa katika zoezi kubwa la utiaji saini mradi mkubwa wa maji kutoka Kiwira,bado tukashirikishwa tena utiaji saini mradi mkubwa wa barabara nne kutoka Nsalaga mpaka Songwe, Sasa hao ndugu zetu wanaotuchafua kuwa tunapinga uwekezaji sisi hatuwezi kuipinga serikali hata siku moja bali tunaiunga mkono kwa asilimia 100, “amesema Chifu Lyoto.
Chifu Malongo Hasara (Mwaigonela)amesema kuwa wanaojiita machifu na kuchafua Mkoa wa Mbeya ,hatutaki watuchonganishe na serikali kabisa tunataka amani na kama hao watu wangekuwa machifu tunaomba wajitokeze.
“Huyo anayezungumza kuwa ni chifu wa mbeya tunaomba ajitokeze hapa leo hii na ikiwezekana akamatwe mara moja kwani huyo mtu anataka kuvuruga Mbeya , sisi hatutaki kuchonganishwa na serikali tunataka amani kama tulivyozoea “amesema.
Katibu Msaidizi wa Machifu Mkoa Mbeya,Mwanauta Ilanga amesema kuwa hawatakubali machifu kuchafuliwa ovyo na watu wanaojiita machifu,tunaaiachia serikali masuala ya uwekezaji hatuwezi kuingilia.
Amesema kuwa wanaheshimu serikali hawawezi kupingana nayo tutabaki kuheshimu na kushirikiana nayo.
More Stories
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo