November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIRDO yaendelea kufanya tafiti za kuchakata taka kuwa bidhaa adhimu

Na Joyce Kasiki,Timesamajira online ,Mbeya

SHIRIKA la Utafiti la Maendeleo ya Viwanda Nchini (TIRDO) limeendelea kuonyesha teknolojia zinazolenga katika utunzaji wa mazingira kwa kufanya tafiti ya vitu vinavyoonekana ni uchafu na kutengeneza bidhaa ambazo zinaweza kukuza soko la ajira hususan kwa vijana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la TIRDO kwenye maonyesho ya Wakulima Nane Nane jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale Mhandisi Paul Kimath kutoka TIRDO amesema,tafiri zilizofanywa na shirika hilo ni za maganda ya chungwa,na kubaini zinatoa mafuta mazuri ambayo yanauzwa kwa gharama kubwa.

Vile vile amesema pia Shiria hilo limeweza kutenegenza mafuta yanayotokana na mchaichai na karafuu ambayo yana kazi nyingi katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuchuo ,kuondoa uchovu lakini pia yanaweza kutumika hata kwa chakula.

“TIRDO tumekuja na teknolojia tatu  ikiwemo ya utengenezaji wa mafuta tete ambayo yanatokana na mimea mbalimbali ,maua na matunda mbalimbali,magome ya miti ,mbogamboga,na moja ya mafuta tuliyotengeneza ni mafuta ya karafuu ambayo baada ya utafiti tumegundua ina mafuta bora na mazuri ,kwa hiyo inachakatwa kwenda kwenye mafuta,

Mafuta hayo ni dawa yanaweza kutumika hata kwenye chakula”amesema Mhandisi Kimath amesema na kuongeza kuwa

“Pia tumekuja na mafuta ya mdalasini,yana ubora wa hali ya juu,tunayo mashine ya kuchakata bidhaa hizo

Pia bidhaa ya mafuta ya maganda ya chungwa ,ni tiba ya mifumo ya hewa,maganda haya ukitembea sehemu nyingi yanatupwa kama takataka na kufanya uchafuzi wa mazingira na TIRDO tukaona hilo ni tatizo kubwa nchini tukaamua kufanya tafiti hiyo kujua jinsi ya kuongeza tathamani ya maganda hayo ya chungwa na kutengeneza mafuta.”

Pia amesema,”Tunafundisha tunatoaushuari tunadizaini  mashine wenyewe ,tunayo mafuta ya mchaichai unaofahamika kama kiungo cha chai lakini TIRDO tunachakata mafuta ya zao hilo.”

Kwa mujibu wa Mhandisi Kimath  ipo miti mingine mingi inayoweza kutoa mafuta kama vile tangawizi huku akiwaasa wananchi wafike katika banda hilo kwa ajili ya kujifunza teknolojia tofauti tofauti za kuongeza thamani ya mazao hasa yale yanayoonekana ni takataka baada ya kutumika kwa bidhaa husika kama vile chungwa na matunda yote ya jamii hiyo.

“Kwa sasa mafuta hayo yanayotokana na bidhaa kama vile chungwa,ndimu, limao hutoa mafuta ambayo yana gharama kubwa ,katika mills 10-15 inauzwa sh 30,000 kwa hiyo utaona jinsi ambavyo bidhaa hizo zina thamani kubwa baada ya kuchakatwa kutoka kwenye matunda hadi kwenye mafuta.”

Hata hivyo Mhandisi huyo amesema,bado wanaendlea na tafiti kwa upande wa matumizi kujua soko kubwa litakuwa wapi ,watu watawekeza vipi, kiasi gani cha mtaji kinahitajika kwa ajili ya kiwanda kidogo vcha kuchakata mazao hayo.