November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rc Mtwara aipongeza Masasi kujenga shule ya mfano

Na Esther Macha, Timesmajira, Online,Masasi

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali ,Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa ujenzi wa shule ya mfano huku akiiagiza kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji muhimu ikiwemo chakula shuleni ili kuona umuhimu wa kupata elimu.

Mwenye skafu ya njano Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed

Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo leo wakati akikagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mkomaindo iliyojengwa kupitia fedha za mradi ya Boost kutokana na shule kongwe ya Mkomaindo kuwa na mrundikano wa wanafunzi.

“Niwapongeze sana kwa mradi huu kwani umejengwa kwa kiwango na kuwa shule ya msingi ya mfano mnastahili pongezi kubwa shule imejengwa kwa viwango na ni mfano tosha,mgema msije kutia pombe maji mkaharibu”amesema.

Amesisitiza na kuwataka walimu kutoa elimu bora ikiwemo mahitaji muhimu ya chakula na mengineyo .

Aidha ameutaka uongozi wa Mji wa Masasi kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwepo na kupewa mahitaji muhimu ili waone kuwa shule si adhabu pia upatikanaji wa chakula uwepo mfano uji wazazi wajitahidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Hashim Namtumba amesema wanamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020.

Amesema ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 inatekelezaka na kwamba wanamshukuru Mbunge wa Jimbo la Msasi kwa mchango wake,madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Masasi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi katika halmashauri hiyo.

Shule ya mpya ya msingi ya Mkomaindo ilipatiwa zaidi ya milioni 331 kwa ajili ya ujenzi huo wenye mkondo mmoja ambapo shule mama ina jumla ya wanafunzi 1,531.