November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCAA yawatoa hofu wananchi kuhusu utafutaji, uokoaji ndege aina ya Embraer 120

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) imewatoa hofu Watanzania kuhusu kuwepo kwa ajali ya Ndege aina ya Embraer 120 iliyokuwa imebeba Abiria 25 iliyoanguka katika kijiji cha msufini kata ya Mbezi wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kuwa haikuma ajali bali lilikuwa ni Zoezi la kujiweka uteyari kwa ajili ya kupambana na majanga ya Ajali za ndege pindi yakitokea.

Akizungumza na waandishi kwa niaba ya Mkurugenzi wa TCAA,Hamza Johari,Afisa uhusiano TCAA,Yessaya Mwakifulefule,kuzungumzia zoezi la utafutaji wa Ndege amesema zoezi hilo lengo lake ni kupima uwezo na utayari kama nchi kukabiliana na matukio ya utafutaji na uokoaji wa ndege zinazopata ajali kwenye nchi kavu au majini na pia vyombo vya majini.

Aidha,Mwakifulefule amesema zoezi hilo limeandaliwa na TCAA,shirika la uwakala wa meli nchini (TASAC),Mamlaka ya Usafiri wa Baharini upande wa Zanzibar(ZMA) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mwakifulefule,amesema zoezi hilo pia limehusisha waangalizi wa Ndani na nje ya nchi ili kutathmini maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili huduma husika itolewe kwa ufanisi mkubwa na waangalizi hao watatoa ripoti ambazo zitafanyiwa kazi na kamati za kimataia

“zoezi hili kwa mwaka huu kauli mbiu okoa maisha ,Tanzania imeridhia mkataba wa kimataifa ya Usafiri wa Anga,Mkataba wa shirika la Bahari Duniani(IMO) pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Anga wa mwaka 1944 ambao kinaeleze kuhusu masuala ya utafutaji na uokoaji”Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce amesema

Flora amesema zoezi hilo lilihushisha taasisi za utafutaji na uokoaji za umma na binafsi zikiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mashirika ya ndege, Mashirika ya vyombo vya majini, Mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA), Mamlaka ya hali ya hewa (TMA), Hospitali, Shirika la msalaba Mwekundu Tanzania (Red Cross), Wavuvi, pamoja wadau wengine mtambuka wa utafutaji na uokoaji ambapo kauli mbiu ya zoezi la mwaka huu 2023 ni “Okoa Maisha” (Save life).

“Tanzania imeridhia Mkataba wa Kimataifa wa Utafutaji na Uokoaji Majini wa mwaka 1979 (International Convention on Maritime Search and Rescue, (SAR Convetion,1979) unazungumzia kuhusu masuala ya utafutaji na uokoaji katika usafiri wa majini.” amesema Flora

Pia amesema mikataba hiyo yote inayosimamiwa na ICAO na IMO inazitaka nchi wanachama kutoa huduma za utafutaji na uokoaji katika usafiri wa anga na majini wakati ajali na matukio ya dharura ya vyombo vya usafiri wa anga na majini ndani ya eneo la nchi mwanachama na wa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, eneo la nchi la utafutaji na uokoaji ni mipaka ya kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na eneo la Bahari ya Hindi kuanzia pwani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mashariki hadi Longitudi nyuzi 44 (440E) pamoja na maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Amesisitiza kuwa katika utekelezaji wa maelekezo yaliyo katika Mwongozo huo, Tanzania imeimarisha na kuboresha vituo vya kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji katika usafiri wa anga na majini ambavyo Vituo hivyo vinavyojulikana kama Aeronautical Rescue Coordination Centre (ARCC) ambacho kipo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na Maritime Rescue Coordination Centre (MRCC) ambacho kipo eneo la Magogoni, Dar es Salaam.

Kituo cha ARCC kinasimamiwa na TCAA na kituo cha MRCC kinasimamiwa na TASAC.

Amesema mwongozo huo wa ICAO na IMO unazitaka nchi wanachama kufanya majaribio au mazoezi ili kupima uwezo na utayari wa taasisi zote zinazohusika katika kutoa huduma hii muhimu ya utafutaji na uokoaji hivyo kufanya mazoezi haya ni kutekeleza matakwa ya sheria na mikataba ya kimataifa ili kuboresha mifumo, taratibu na vifaa vya utafutaji na uokoaji.