December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Chalamila atangaza ujio wa wakuu wa nchi mbalimbali Dar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari ujio wa wakuu wa nchi mbalimbali kwenye mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu rasilimali watu utakaofanyika tarehe 25-26 kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere- JNICC Dar es Salaam.

RC Chalamila amesema Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndio mwenyeji wa mkutano huo mkubwa ambapo wakuu wa nchi za Bara la Afrika kuja na Azimio la kujenga Afrika mpya yenye kuzingatia mahitaji ya Rasilimali watu kama ilivyo kuwa Falsafa ya Rais wa kwanza wa Taifa hili Mwl JK Nyerere alisema “Ili tuweze kendelea tunahitaji vitu vinne Watu , Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora” watu wenye ujuzi na weledi, Azimio la Dar es Salaam lina kwenda kujenga na kutathimini mambo ya kuzingatia ili kufikia mwongozo wa Bara la Afrika lenye watu wenye thamani ya kuendeleza Bara hili.

Adha RC Chalamila amesistiza kuwa Ugeni huu ni Jiji la Dar es Salaam Jiji la maraha ambalo Afrika inalitumia katika kuhakikisha Azimio juu ya ufanyaji kazi wa kizazi cha Afrika unaimarika kwa manufaa ya Bara la Afrika, Tanzania ni nchi ya mfano kwenye mambo mengi hivyo hatuna budi kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada yake katika kukuza uchumi na kujenga taswira nzuri ya nchi yetu ndani na nje ya nchi.

Vilevile ni ukweli usiopingika toka Rais Dkt Samia aingie madarakani amewekeza nguvu kubwa kujenga taswira nzuri ya nchi na matunda yake ndio haya tunaona ya kufanyika kwa mkutano mkubwa wa wakuu wa nchi Bara la Afrika kuhusu Rasilimali watu.

RC Chalamila amesema Mikutano hii ni Sehemu ya Utalii na ujio wa wageni ni muhimu katika kujenga utalii wa mahoteli, fukwe na vyakula vya Kitanzania, kutakuwa na wageni wasiopungua 1,200 watakao lala, kula vyakula na kutembelea maeneo mbalimbali hivyo tuitumie vizuri fursa hii.

Hata hivyo RC Chalamila amesema lengo kuu la Serikali ya Mkoa ni kuhakikisha wageni wanaacha Dola hapa hivyo tumeanda maeneo maalum ambayo wafanyabishara na wajasiriamali wataweka bidhaa zao kwa ajili ya kuuza katika eneo la nje la Ukumbi wa JNCC.

Sambamba na hilo RC Chalamila amewataka wakazi wa Jiji hilo kuendelea kuliweka Jiji safi, pia ameeleza sababu ya Benki ya Dunia kuridhia mkutano huo mkubwa kufanyika Tanzania- Dar es Salaam ni kutokana na Amani iliyoko, kuwepo kwa vijana wengi wasio na ajira kama ilivyo kwa nchi nyingine za Africa hivyo watajifunza namna nchi inavyokabiliana na Changamoto na Utaoji wa elimu bila malipo kwa Shule za msingi na Sekondari kama mkakati wa kuzalisha wataalam nalo watajifunza.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Ndg Ephraim Mafuru amesema hadi kufikia leo Julai 21, 2023 maandalizi yote muhimu yamekamilika katika nyanja zote kumbi na vifaa vyote muhimu viko tayari.