Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Shirika lisilo la Kiserikali AMO FOUNDATION inatarajia kugawa pikipiki kwa Vijana na Vyerahani Agosti mwaka huu Ili kuwawezesha vijana kwa ajili ya kutambua mchango wa vijana wa Taifa hili.
Mkurugenzi wa AMO FOUNDATIO Amina Said ,alisema shirika hilo linatarajia kufanya kongamano lenye lengo la kutambua vijana Agosti mwaka huu lengo la kufanya uwezeshaji kwa viajana ,Wanawake ,watoto na watu wenye mahitaji maalum katika kuendeleza shughuli zao.
” Amo Foundation ipo Tanzania nzima mikakati yetu tutagawa Bodaboda na Vyerahani kwa kuanzia Mkoa Dar es Salaam baadae katika mikoa mingine Kijana na Kazi ”
Kauli mbiu uwajibikaji wetu ndio uhai wa uchumi wetu.
” tukio hili Maalum la uwezeshaji kwa Vijana wajasiriamali kutoka katika makundi ya Bodaboda ,makonda wa Daladala ,Machinga wauza chakula (chips) Wanafunzi wa vyuo na makundi mengine ” alisema Amina .
Mkurugenzi Amina Said ,alisema kwa kutambua mchango mkubwa wa serikali wa awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa bajeti ya mwaka 2022 /2023 amechangia shilingi bilioni 1.88 ambayo imetolewa na kama mikopo ya uwezeshaji kiuchumi vijana katika sekta ya kilimo viwanda na Biashara.
Alisema katika Kongamano hilo Mgeni anatarajia kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi vijana, ajira, na wenye ulemavu ).
Patrobas KatambiAidha alisema pia serikali imetoa Mafunzo ya ujasiriamali ,usimamizi wa fedha ,urasimishaji na kuendeleza Biashara katika mikoa mbalimbali nchini na wameshudia katika mwaka 2022 /2023 ikiendesha oparesheni za kuwakamata wanaojoushisha na Biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kuzui mianya ya kusafirisha na kusambaza Dawa hizo Ili kuepusha kundi kubwa la vijana ambalo nguvu kazi ya Taifa Alisema vijana watapata nafasi ya kujifunza mambo mbali mbali kama kujitambua ,Biashara na uwezeshaji, masoko umuhimu wa kutii sheria za nchi na fursa zinazopatikana nchini .
” Shirika la Amo Foundation tunaendelea kututambua jitihada hizi za vijana tumeweka mikakati ya uwezeshaji wa kundi kubwa la vijana kwa lengo la kutatua changamoto za ajira zinazolikabili Taifa na Dunia kwa ujumla ” alisema .
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua