November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dereva bajaji mikononi mwa Polisi tuhuma za ubakaji,shambulio la aibu kwa mwanafunzi

Na Moses Ng’wat,Timesmajira Online, Songwe.

JESHI la Poisi Mkoa wa Songwe linamshikilia dereva wa bajaji Ayubu Mng’osi (30) Mkazi wa Ichenjezya,Wilayani Mbozi kwa tuhuma za ubakaji na shambulio la aibu kwa watoto wadogo wawili wenye umri wa miaka 7 na 9 ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 18, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema kuwa, katika tukio la kwanza, mtuhumiwa huyo anadaiwa kumwingilia kimwili mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Ichenjezya (jina limehifahiwa).

“Mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumlaghai mtoto na kuingia naye ndani ya nyumba anayoishi ambako ni jirani na wazazi wa mtoto kisha kutekeleza unyama huo,”amesema Kamanda Mallya.

Aidha, Kamanda Mallya amesema kuwa mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kumfanyia shambulio la aibu la kumshika na kumchezea sehemu za siri mtoto mwingine ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Ichenjezya (jina limehifadhiwa).

“Julai 14 mwaka huu huko katika maeneo ya Mianzini kata ya Ichenjezya, bibi aligundua kushikwa, kuchezewa sehemu za siri maeneo ya makalioni kwa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la pili na Ayubu Mng’osi,” alieleza Kamanda Mallya.

Kamanda Mallya ameeleza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mthumiwa huyo amekuwa akijhusisha na vitendo kwa nyakati tofauti tofauti na mbinu alizotumi ni kuwaingiza watoto hao ndani kwake na kuwafanyia vitendo hivyo vya kinyama.

Amesema jeshi hilo linaendelea kumshikilia mtuhumiwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani ili kupambana na mkono wa sheria.