Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online, Handeni
Kampuni ya bia ya Serengeti,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Handeni (HTM) pamoja na Taasisi ya Water Aid wameshirikiana katika ujenzi wa mradi wa bwawa la maji la Kwamaizi lililogharimu kiasi cha milioni 419.
Utekelezaji wa mradi huo ulihusisha usanifu na ujenzi ambapo bwawa hilo lina ujazo wa zaidi ya mita za ujazo 137,000 na lina uwezo wa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2,000.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi huo,Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi,ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti na taasisi ya WaterAid kwa kushirikiana kupeleka Maji Safi na Salama kwa wananchi.
Mhandisi Mahundi,amesema taasisi hizo zimekamilisha ujenzi wa mradi huo ndani ya miezi mitano ambapo huku akiipongeza RUWASA Mkoa na MD- HTM kutokana na usimamizi mzuri wa mradi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Adv Albert Msando, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Reuban Kwagilwa, viongozi wa Chama cha Mapinduzi, wadau wa sekta ya maji pamoja na wananchi.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â