November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Magembe:endeleeni kuwajengea uwezo wataalamu walio ngazi ya msingi

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameutaka uongozi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu walio katika ngazi ya msingi kwa lengo la kuwaongezea ujuzi katika kutoa huduma bora.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Dkt Grace Magembe

Aidha Dkt .Magembe ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Mbeya ambapo amesema uongozi wa hospital na watumishi kwa kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya, tunaona jinsi wananchi wanavyowapongeza,pia tunaona utayari na uharaka wenu tunapowaletea changamoto za wananchi huwa mnakuwa wepesi kuzitatua ,” Dkt. Grace Magembe.

Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt.Godlove Bwanji

Amesema kuwa pamoja na kazi kubwa wanayofanya bado wana jukumu la kuzijengea uwezo hospitali za wilaya na vituo vyote vilivyoko katika ngazi ya msingi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya kwa uboreshaji wa miundombinu , vifaa tiba ikiwemo mashine ya MRI na kuhaidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoelekeza Dkt. Magembe.

“Tutaendelea kushirikiana na wenzetu, sisi kama hospitali ya Kanda Mbeya, ni wajibu wetu kuwajengea uwezo hospitali za Wilaya na ngazi ya msingi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora,” Dkt. Godlove Mbwanji.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Grace Magembe akiwa na baadhi ya uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wakati akitembelea majengo ya hospitali hiyo

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo huduma za mionzi na huduma za vipimo vya MRI pamoja na huduma za afya ya mama na mtoto.