Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
NAIBU Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema,viongozi wa Dini hapa nchini wanao wajibu wa kuhakikisha wanazungumza suala la malezi bora na makuzi ya watoto kuanzia kwenye uchumba mpaka kwa wasimamizi wa ndoa ili kujenga uelewa wa kutosha juu ya malezi na hatimaye kuondoa ukatili kuanzia kwenye ngazi ya familia.
Aidha Wakili Mpanju amesema,suala la malezi na makuzi ya watoto liangaliwe namna ya kuingizwa kwenye mitaala ili lijengeke kwenye jamii na kutekelezwa ipasavyo na hatimaye kuwa Taifa bora na lenye tija.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Taifa wa wadau wa Malezi na Kutokomeza Ukatili dhidi ya watoto uliofanyika jijini Dodoma.
“Suala la malezi ndiyo limekuwa likichangia hasa katika ukatili dhidi ya watoto,lakini pia suala la utandawazi nalo linachangia,watoto wanaiga mambo yasiyofaa,na wazazi nao wanakuwa ‘busy’ na mambo yao hawana hata muda wa kuzungumza na watoto ,kwa hiyo mtoto anaanza kufanyiwa ukatili kidogo kidogo mwisho wa siku mpaka mzazi anakuja kugundua wakati mtoto maeshaharibika,
“Kwa hiyo katika hili ni vyema viongozi wa dini zote waingilie kati suala hili ili waweze kuzungumza na wazazi na walezi tangu wakati wa uchumba,wale wasimamizi wa ndoa nao waangaliwe wawe ni wale wenye maadili mema ambao wanaweza kutoa ushauri mzuri kuhusu la malezi hata panapokuwa na mgogoro katika ndoa waliyoisimamia na kurejesha utulivu,sasa kama msimamizi ndoa yake inamshinda hivi ataweza kushauri mgogoro wa ndoa?”alihoji Wakili Mpanju
Vile vile amesema,huu siyo wakati wa kuchagua msimamizi wa ndoa kwa kuangalia namna anavyofanana na bibi au bwana harusi na badala yake wasimamizi wanapaswa kuwa wenye maadili mema.
Aidha amesema ,kumekuwa na matukio mengi ya ukatili ambapo takwimu zinaonyesha matukio mengi ya ukatili dhidi ya watoto yamekuwa yakitokea nyumbani mahali ambapo palitarajiwa kuwa pa kwanza kwa usalama wa mtoto.
“Taifa lina changamoto mmomonyoko wa maadili, ukatili dhidi ya watoto unaongezeka tunaweza kuzitumia Taasisi za Elimu Kuja na kuweka mkakati kwenye eneo Malezi kwa kuimarisha na kumuandaa mtoto tangu akiwa Mdogo Ili watu wajue wana wajibu katika suala zima la malezi na usalama wa mtoto ili aweze kukua vyema.”amesema Wakili Mpanju na kuongeza kuwa
“Kuna kufeli Kwa kushindwa kufanya kazi kwa Mifumo ya Ustawi wa Jamii, kuna migogoro ndani ya familia ambayo kwa namna fulani inaathiri kizazi cha sasa na kijacho, madhara yake ni kupata watu ambao wamelelewa isivyo stahili”
Kwa mujibu wa Wakili Mpanju, muelekeo wa serikali ni ulinzi wa mtoto kwa sababu kila mtoto sasa hivi ni muhanga wa ukatili.
Amesema,Taarifa ya utafiti uliofanywa na Serikali na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) ilionyesha asilimia kubwa ya vitendo vya ukatili vinafanyikaa majumbani na wazazi, ndugu jamaa au marafiki ambao wanaoizunguka familia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mwaka 2022 ni 12163, kati ya hivyo vitendo vilivyoongoza ni ubakaji 6335, vinafuatiwa na ulawiti ni 1557, watoto kupewa mimba katika umri mdogo 1555 huku akisema,hivi ssaa kuna kiwango cha ukatili kuongezeka kwa watoto wote wa kike na wa kiume.
“Asilimia 60 ya ukatili wa watoto vinafanyikia nyumbani na asilimia 40 inaoyesha Vitendo hivyo vinafanyikia nje ya nyumbani ikiwemo pia mashuleni, njiani watoto wanapokwenda shule” amesema na kuongeza kuwa
“Lazima kama Taifa tuje na mikakati ya kutokomeza ukatili huo kwa kueneza elimu kwa jamii kwani tusipowekeza katika hilo na kuwasimamia watoto na kuwaelimisha mapema, inaleta athari kubwa kwa watoto wenyewe na Taifa kwa ujumla .”
Awali Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mtoto bw.sebastian kitiku amesema changamoto kubwa waliyonayo wazazi katika malezi inatokana na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo inawapelekea wazazi washindwe kuwalea watoto vizuri.
Amesema kutokana na hilo wao kama serikali wameamua kuja na muongozo utakaowaongoza wadau kuteeleza afua za mtoto ‘Mwongozo wa Taifa wa wajibu wa wazazi na walezi katika malezi ya watoto na familia’.
Hata hivyo amesema,katika kuhakikisha afua za malezi ya watoto zinatekelezwa ipasavyo na Taifa kuwa na watu wenye tija,Serikali na wadau wanatekeleza Programu ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na maendeleo ya Awali ya Mtoto inayowalenga watoto wenye umi kuanzia sifuri hadi miaka minane kwa lengo la kuhakikisha anakua vizuri.
“Moja za afua zinazotekelezwa ni pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto,maana lazima mtoto huyu alinde ili aweze kukua vyema,na kitaalam asilimia 90 ya ubongo wa mtoto unakua katika kipindi cha miaka sifuri mpaka minane,hapa ndipo mahali tunapoweza kupata watoto watakaokuwa na tija kwenye Taifa kwani wamelelewa na kukua katika utimilifu wao.”amesema Kitiku
Akizungumza na mtandao huu,Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania Edda Mbwambo amesema,kama viongozi wa dini wanayo nafasi ya kutoa elimu ya malezi kwa wanandoa katika kipindi cha mafundosho ya ndoa na wamekuwa wakifanya hivyo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi