Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imekutana kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ofisi mpya ya chama hicho.
Katika kikao hicho Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya,Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kushirikiana na Mbunge wa Lupa ,Masache Kasaka wameahidi kuchangia kiasi cha milioni 25(ishirini na tano) kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo.

Huku Madiwani wa kila Kata kuchangia kiasi cha milioni mbili ili kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya chama itakayokuwa na ukumbi wa mikutano sambamba na ofisi za jumuiya zote za chama.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chunya Noel Chiwanga na kuhudhuriwa na Kamisaa wa Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Mayeka Simon Mayeka.
More Stories
Simbachawene:Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji Rasilimaliwatu umebaini upungufu wa watumishi 441,366
Wakazi Arusha watakiwa kuchangamkia fursa huduma jumuishi za kifedha
Wahitimu wa Mafunzo ya Scout Nkasi watakiwa kuwa mwangaza kwa vijana