November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mapinduzi makubwa miaka 60 ya NIC

Na Penina Malundo,Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa NIC Insurance Dkt.Elirehema Doriye amesema miaka 60 ya NIC Insurance ni mapinduzi makubwa yamefanyika katika kutoa huduma za bima nchini.

Dkt.Doriye ameyasema hayo kwenye banda la NIC Insurance kwenye maonesho ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema safari ya miaka 60 ilikuwa ya mabonde na milima lakini mapinduzi makubwa yamefanyika katika NIC kutumia ubunifu kwenye mapinduzi ya teknolojia kwa kutengeneza mifumo ya Kidijitali ya kuwafikia kiurahisi na kufanya huduma zetu kuingia sokoni na kupokelewa kiurahisi.

Amesema katika mapinduzi ya Teknolojia NIC imeweza kupata Tunzo ya Superbrands Afrika Mashariki ambapo makapuni mengine hayajafikia tunzo hiyo.

“Mafanikio yetu yanatokana na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua mipaka ya uwekezaji na biashara na kufanya NIC Insurance kupita katumia mipaka hiyo iliyofunguliwa na Rais Wetu”amesema Dkt.Doriye.

Amesema kuwa kasi yao haitaishia hapo kwani watanzania wanaitegemea NIC katika kuwafikia kutoa huduma za bima ili waweze kujenga uchumi ambao hata majanga yakitokea NIC kuwashika mkono kutokana na bima zao.

Aidha amesema kuwa miaka 60 hiyo kwao ni sehemu ya deni kwa watanzania katika kuhakikisha wanawafikia katika makundi yote na kuwa NIC Insurance ni kimbilio la huduma bora za bima.

Amesema kuwa NIC Insurance imekwenda mbali hadi kupata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kutoa huduma bora kwa wateja

” NIC Insurance naendelea kuboresha huduma kwa viwango vya Kimataifa kwa sababu wanauzoefu katika bima wataendelea kuwa bora zaidi,”amesema.