Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) kuanza ujenzi wa nyumba 200 za makazi katika jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya mpango wa Shirika hilo kuwezesha makazi bora kwa Watanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah amesema Kwa mwaka huu wa fedha tunaanza ujenzi wa nyumba 100 katika eneo la Njedengwa ikiwa ni awamu ya kwanza ya Mpango wa Samia Scheme kwa Jiji la Dodoma
Pia Shirika litaanza ujenzi wa nyumba 100 katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba, nyumba hizo zitakazoanza kujengwa ni nje ya zile 300 zilizokamilika Iyumbu na zingine 100 za Chamwino, Dodoma.
“Hii ni katika kutimiza azma ya kufikisha nyumba 5,000 Tanzania nzima , tunakwenda Dodoma, lakini huenda tukaanza awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 500 pale Kawe hata kabla hatumalizia hizi nyumba 560 zinazokamilishwa sasa,” amesema.
Shirika la Nyumba la Taifa ni miongoni mwa Mashirika na makampuni 1, 188 ya ndani yanayoshiriki maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba na zaidi ya Mataifa 30 duniani, yanatarajiwa pia kushiriki katika maonesho hayo ya mwaka 2023.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â