December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospital Segerea kufungua shule ya famasia, uuguzi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Hospitali ya Miracolo iliyopo Segerea Wilaya Ilala imejipanga kufungua shule ya Pharmacy na uuguzi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Miracolo, Deogratias Kweka, wakati wa hafla fupi ya miaka saba ya hospitali hiyo.

Kweka alisema mikakati hiyo ya Miracolo inatarajia kufanyika katika malengo yake waliojiwekea katika kuunga mkono Juhudi za Serikali.

“Miracolo ni hospitali ya kisasa ina madaktari bingwa wa watoto inatibu magonjwa yote na oparesheni zote zinafanyika.Mikakati yetu ya upanuzi wa hospitali tutajenga shule ya kisasa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Pharmacy na wauguzi,” alisema Kweka.

Naye Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye ni Mlezi wa hospitali hiyo, Dkt. Hamis Kigwangala, amepongeza mafanikio ya hospitali hiyo ilipofikia na kumtaka mkurugenzi kuwa na mikakati ya maendeleo.

Dkt. Kigwangala amewataka Miracolo washirikiane na vituo vya afya vingine pamoja na hospitali zingine ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Miracolo, Dkt. Anna Deogratias, amesema malengo ya hospitali hiyo ni kuongeza huduma za kibingwa katika kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya.

Dkt. Anna amesema hospitali hiyo ina madaktari bingwa wa kisasa inatibu magonjwa yote ya watoto na inafanya operesheni magonjwa yote hivyo imekuwa mfumbuzi wa matatizo ya afya.

Amesema malengo mengine waliyojiwekea ni kuishi kwa kushirikiana na vituo vya afya vinavyowazunguka ili kuokoa maisha ya wagonjwa pindi wanapofika kufuata matibabu.