Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
YANGA imetangaza bajeti ya Tsh 20.8 bilioni kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya ndani ya nchi [Ligi Kuu, Kombe la Azam Sports Federatio] pamoja na mashindano ya kimataifa [CAF].
Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga, Sabri Sadick amesema kupitia bajeti hiyo anaamini italeta tija kwa klabu kwa msimu ujao na kufanya vizuri zaidi.
Kwenye vyanzo vyetu tuna Tsh. 14.8 bilioni, kwa hiyo tuna upungufu wa Tsh. 6 bilioni ambazo tunafanya jitihada za haraka kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali tuweze kufikia malengo.
Sadick amesema bajeti ya msimu ujao ni zaidi ya msimu uliopita ambapo Yanga ilitumia Tsh. 17.3 bilioni huku bajeti ikiwa ni 17.8 bilioni hivyo kubakiwa na Tsh. 581 milioni.
Kwa mijibu wa Sadick, ongezeko la bajeti kwa msimu ujao ni kwa sababu ya kuongeza ufanisi zaidi kwa klabu ya Yanga.
Sadick amesema bajeti ya msimu uliopita ilitokana na fedha za wadhamini mbalimbali wa klabu, mauzo ya jezi, mauzo ya wachezaji, viingilio vya mechi, ada za wanachama, mikopo na mapato mengine.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa