November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chongolo:Zalisheni zabibu ya mwisho msiishie kwenye mchuzi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Chamwino.

WIZARA ya Kilimo imetakiwa kwenda mbali zaidi katika suala la kilimo cha zabibu katika masoko wazalishe zabibu ya mwisho na siyo kuishia kwenye mchuzi ili kuuza nje ya nchi.

Hayo yamesemwa Wilyani hapa leo,Juni 18,2023 na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)alipotembelea mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Jenga Kesho Bora uliopo Chinangali Wilaya ya Chamwino na Mashamba ya ushirika wazabibu .

Ambapo amesema kuwa Wizara ya kilimo iangalie namna ya kuzalisha zababu ya mwisho ili mfanyabiashara biashara mdogo aweze kuweka blandi yake ili ifahamike na kuuzwa nje ya nchi kama ambavyo wine za nje zinavyouzwa Tanzania.

“Nimewasikia hapa mkizungumzia mipango na mambo mengine makubwa niseme tu nilazima tuache kufikiria mnunuzi wa zabibu yetu kutoka nje ya hapa lazima matazamo uwepo kwa uzalishaji wa zabibu ya mwisho hapa ambayo tukiiblandi inaenda kuwa na jina Dunia nzima wenzetu ndiyo wanachofanya,

“Ukifikiria wine inayoingia nchini ndiyo inakupa sura ya kiwango matumizi ya wine ndani ya nchi yetu na nyinyi mnapaswa kuangalia asilimia ngapi ya hiyo wine inayonyweka nchini kutoka ndani ya uzalishaji wa ndani maana yake ni kidogo sana kwahiyo kwa soko tu la ndani muweke nguvu,”amesema Chongolo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde amesema kuwa changamoto kubwa ya wakulima wa zabibu ni masoko hivyo wao kama Wizara wanampango wa kuwakomboa wakulima katika soko la zabibu .

Amesema kuwa Kwasababu sasa hivi wachakataji wengi wanashindwa kuchakata matenki yao yamejaa tunazungumza wamezungumza na TBL na kukubaliana kusaidia katika upatikanaji wa mchuzi wa zabibu kwasababu ndiyo inayofanya wine nyingi ibaki kwenye matanki.

Aidha amesema watahakikisha wanaongeza kodi katika wine ambayo inaingia nchini kutoka nje ili kulinda viwanda vilivyopo nchini.

Pia amesema wanamtafuta mnunuzi mwingine ambaye anaweza kununua ukiacha wanunuzi wa zamani ambao kina jambo kutoka shinyanga ambaye hatengenezi mvinyo na kwa mara ya kwanza ameanza kutengeneza juisi kupitia tunda la zabibu.

“Wakulima wengi zabibu zao zinaoza shambani kwasababu hawana uwezo mkubwa wa uhifadhi wa zabibu kwahiyo serikali tumeanza kama mfano kiwanda cha kuchakata zabibu na mwaka wa fedha unaokuja tunawawezesha wakulima zabibu zao kupata soko”amesema.

Naye Waziri Mkuu na Makamo wa kwanza wa Rais Mstaa ambaye ni mhasisi wa mashamba ya ushirika wa zabibu,John Malecela ametoa wito kwa wenyeji wa mkoa wa Dodoma waone umuhimu wa kuingia kwenye zao la zabibu na kulitekeleza vizuri kwasababu litafadhiri hali ya maisha yao.

“Mimi ni mhasisi wa mashamba haya pia natania watu nasema sisi ndiyo wenye nchi kuna wananchi na wenye nchi kwahiyo tupo kwenye miradi hii ilikuonesha muungano kati yetu na wananchi wetu zao la zabibu katika Dodoma ni moja wapo ambayo inakitu kimoja ambacho ni tofauti kwamba katika ulimwengu mzima kuna nchi mbili tu ambazo zinaweza kutoa zabibu kwa mwaka mara mbili na Tanzania ni hapa Dodoma huwa tunavu a mwezi wa tatu na wasaba,”amesema.